TreasureFred
Member
- Feb 25, 2008
- 64
- 3
Inatia shaka ujenzi wa Barabara 4 wakati kwingine hakupitiki kabisa huku mazao yakiozea shamba kwa sababu ya miundo mbinu mibovu
Wana JF, mbunge wa Nzega leo ametoa kauli kali pale aliposema kuwa serikali inatumia pesa bila idhini ya bunge na pia kuwashutumu mawaziri kuwa wana hila na hawana nia njema na wabunge
Katoa mifano kuwa barabara ya Chalinze serikali imetumia fedha bila ruhusa ya bunge na kuwaambia mawaziri watalaaniwa na kama hawajui kifo waangalie makaburi.
Kama kawaida yake, Selelii amewawashia moto mawaziri kwelikweli.
[/SIZE] Baada ya kumaliza kuchangia kuna mbunge mmoja wa kutoka Tanga nadhani ni Rished Abdalla akaomba mwongozo wa spika kwamba Selelii ametumia lugha ya kuudhi/kukera kwa kuwaambia mawaziri Mungu atawalaani. Spika akaimaliza kiutu uzima.
Kwa kweli Selelii ni aina ya Wabunge ambao Tanzania inawahitaji ili iendelee.Hivi kweli kila anakuwa kiongozi anafikiria kuendeleza kwao tu,kweli tutafika?
Wana JF, mbunge wa Nzega leo ametoa kauli kali pale aliposema kuwa serikali inatumia pesa bila idhini ya bunge na pia kuwashutumu mawaziri kuwa wana hila na hawana nia njema na wabunge
Katoa mifano kuwa barabara ya Chalinze serikali imetumia fedha bila ruhusa ya bunge na kuwaambia mawaziri watalaaniwa na kama hawajui kifo waangalie makaburi.
Kwakweli ukiangalia huu utaratibu wa vipaumbele vya miundombinu unashindwa kuelewa mipango ya serikali. Kama alivysema selelii kuna mantiki gani kupanua barabara ya chalinze segera badala ya chalinze dar?manake kuanzia chalinze kwenda dar ndio kuna traffic kubwa, magari toka kanda ya magharibi, nyanda za juu kusini na kanda ya kati.Halafu kuna maneno mitaani eti mawaziri wanajipendelea maeneo yao; wengine wanasema viongozi wa serikali wanajipendekeza kwa JK. Tumesikia leo kwenye vyombo vya habri kuwa wabunge wa morogoro wamejipanga kwa dhati kumtetea Mkulo, sasa hapa ndio tunapogundua kwamba hizi bajeti wamezipanga kwa kujipendelea.Kwanini watu wateteane kwa kanda/mikoa wanayotoka? Sie walima dhahabu nyeupe iliyo juu ya ardhi tutaendelea kula vumbi tu kama kawaida huku wengine wakibadilisha lami kila mwaka.
Kuna mtu mmoja alisha leta hoja ya siasa za ukanda/majimbo hapa JF, kwamba zipo na zinaendelea, nilijitahidi kumpinga kwa nguvu zangu zote.. ila kama hili lipo akili yangu ina nirejesha mara moja katika hoja ya yule jamaa niliye mpinga mno!