Mh Selelii awaambia mawaziri wana hila bungeni na hawawatakii mema wabunge

Mh Selelii awaambia mawaziri wana hila bungeni na hawawatakii mema wabunge

Ningekuwa na uwezo 2010 mzee Six angechukuwa urais tuongeze nguvu ya kupambana na ufisadi, maana huyu mzee amekuwa akiwapa support nzuri sana wabunge wanaothubutu kusema ufisadi hadharani.
Ingekuwa enzi za Mkapa ungesikia kikao cha wabunge wa CCM kinaitishwa watu wakatishwe ili kuufyata....hata Selelii alikuwa akiufyata.
 
Fedha za ujenzi wa bara bara 4 zingetumika ktk kuongeza jitihada za kuipatia tanzania umeme wenye kuwa na uhakika.!!
 
Sisi "political Analysts" tukiona matumizi ya pesa yanafanyika hata bila idhini ya Bunge kwa kipindi ambacho bado takribani mwaka mmoja tu kufikia uchaguzi moja kwa moja tunapata wazo kuwa mambo hayaendi sawa kwa baadhi ya waheshimiwa, hivyo wanataka kuharakisha mikakati yao ya kudanga wapiga kura kuwa wamewajibika. Wizi Mtupu.
 
Alichosema Seleli ni kweli tupu na ni mfano mzuri wa kongozi ambaye anaguswa na masuala ya jamii. Yupo pia Siraju Kaboyonga. Nimekuwa nikimsikiliza kwa makini sana kuhusu namna anavyochambua masuala ya msingi ya kiuchumi na kutoa mwongozo. Angesikilizwa tungepata mwelekeo mzuri. wanachosema wabunge hawa ni nini. Katika kipindi hiki cha kuanguka kwa uchumi ambapo uchumi wetu unatarajiwa kushuka kwa asilimia 2 kutoka 7 tulizofikia, kuna kila sababu ya kutafuta njia za msingi za kuhakikisha kuwa hatutetereki zaidi. baadhi ya njia hizi ni kuimarisha miundo mbinu ya ndani ili irahisishe usafirishaji wa bidhaa na kufungua maeneoe zaidi ya kiuchumi ili yachochee ukuaji wa uchumi. Kuunganisha barabara Kuu na kuimarisha usafiri wa reli ingekuwa ni wazo la kwanza. Lakini pia kutazama barabara ambazo zinaingia kwenye maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya utalii. Nitoe mfano mdogo tu. Kutoka Iringa Mjini hadi Ruaha Natioanl Park ni Km. 126 ambazo ni sawa na mwendo wa saa 1:15 kama barabara hiyo ingekuwa ya lami. lakini kwa sasa ili uende huko ni lazima utumie saa 3:00. Hii imefanya Hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa Tanzania kwa vipindi fulani fulani kukosa kabisa watalii wa ndani na nje. Vile vile katika uchumi duni kama wa Tanzania moja ya vitu ambavyo hupandisha gharama ya maisha ni chakula. Hivi sasa mikoa ya Kaskazini na kati kama manyara, arusha, Singida na Dodoma ina matatizo makubwa ya chakula. Lakini kuna chakula cha kutosha katika mikoa ya nyada za juu kusini(Iringa, Mbeya, Ruvuma na Rukwa) hivyo kama barabara ya Iringa - Dodoma ambayo ina Km 240 hivi ingekuwa imetengenezwa kwa kiwango cha lami ingekuwa rahisi sana kusafirisha chakula hicho. Hivi sasa ni lazima upite Morogoro ndipo urudi Dodoma. Hii ni mifano michache juu ya namna tusivyotambua nini tunatakiwa kufanya na kwa wakati gani.
 
Kujipendekeza pendekeza kwa wabunge wengi pia kunaharibu maana ya bunge. Mbunge akitoa hoja ya maana kwa kutumia busara, hekima na ujasiri alivyopewa na MUNGU kama vile Mh. Selelii, wanaanza kumshambulia. Mbaya!!. Watanzania inabidi tuanze kubadirika, wabunge kama hao ni kuwapiga chini tu uchaguzi ujao, wanakera!
 
Mpoki, uko sahihi lakini nani amsikilize Mh. kama Siraju Kaboyonga maana wengi wako bungeni kuangalia machungio yao yasivamiwe na "nguruwe" pori. Level ya selfishness ni kubwa sana miongoni mwa waheshimiwa wetu. Kama ingekuwa ni cancer wengi wako level ya beyond treatment.
 
Jamani Tanga kuna bandari.... mnataka wajenge barabara yakwenda hewani? Tuongezeni capacity ya bandari zetu and related infrastructure... Huko kwingine tule udongo kwanza for a while..
 
Sijui Serikali itamjibu namna gani Mheshiwa Spika Sitta ili Mhe. Selelii aridhike.

Lakini sisi Watanzania ni vema tukatambua kuwa ni omba omba wa kutupwa! Kama Denmark imetupa fedha baada ya kupokea ombi letu na kuona tuna shida ya barabara ya Chalinze-Segera, na kwamba ktk Bunge lake huko Denmark, fedha hizo ni lazima zitumike au ziwe "committed" kabla ya June, 2009, basi ni lazima sisi tukubali, hata kama wakina Selelii wangetaka kupitisha "makubaliano" yao. A beggar cannot choose!!! And above all, this is only a question of timing, not a question of where the grant from the donor will go.

By being so beggarly, we as a country have compromised our sovereignty and independence in deciding on so many things that take place in this land. The solution is not to play delaying tactics, but moving positively fast forward with projects which can facilitate genuine development for all of us.
hii ya kutumia mgongo wa donors ni kuficha uchafu au ukweli., donors huwa anaombwa kufadhili barabara kufuatana na priority zako, sasa ikiwa mimi ninatoka mtera na labda ni waziri wa fedha au wa miundo mbinu , basi nitampa somo donor kumuonyesha umuhimu wa hiyo barabara, basi akiridhia ndio hivyo tena yanakuja ya wengine why not this road or that road. tunachotakiwa ni ile tume ya uchumi, kuwa inapitia projects zote za nchi na kupanga priority zetu kwama ikitokea fedha za donor ama za ndani basi mradi huu ndio wa kuanza then huu etc etc.
 
Alichosema Seleli ni kweli tupu na ni mfano mzuri wa kongozi ambaye anaguswa na masuala ya jamii. Yupo pia Siraju Kaboyonga. Nimekuwa nikimsikiliza kwa makini sana kuhusu namna anavyochambua masuala ya msingi ya kiuchumi na kutoa mwongozo. Angesikilizwa tungepata mwelekeo mzuri. wanachosema wabunge hawa ni nini. Katika kipindi hiki cha kuanguka kwa uchumi ambapo uchumi wetu unatarajiwa kushuka kwa asilimia 2 kutoka 7 tulizofikia, kuna kila sababu ya kutafuta njia za msingi za kuhakikisha kuwa hatutetereki zaidi. baadhi ya njia hizi ni kuimarisha miundo mbinu ya ndani ili irahisishe usafirishaji wa bidhaa na kufungua maeneoe zaidi ya kiuchumi ili yachochee ukuaji wa uchumi. Kuunganisha barabara Kuu na kuimarisha usafiri wa reli ingekuwa ni wazo la kwanza. Lakini pia kutazama barabara ambazo zinaingia kwenye maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya utalii. Nitoe mfano mdogo tu. Kutoka Iringa Mjini hadi Ruaha Natioanl Park ni Km. 126 ambazo ni sawa na mwendo wa saa 1:15 kama barabara hiyo ingekuwa ya lami. lakini kwa sasa ili uende huko ni lazima utumie saa 3:00. Hii imefanya Hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa Tanzania kwa vipindi fulani fulani kukosa kabisa watalii wa ndani na nje. Vile vile katika uchumi duni kama wa Tanzania moja ya vitu ambavyo hupandisha gharama ya maisha ni chakula. Hivi sasa mikoa ya Kaskazini na kati kama manyara, arusha, Singida na Dodoma ina matatizo makubwa ya chakula. Lakini kuna chakula cha kutosha katika mikoa ya nyada za juu kusini(Iringa, Mbeya, Ruvuma na Rukwa) hivyo kama barabara ya Iringa - Dodoma ambayo ina Km 240 hivi ingekuwa imetengenezwa kwa kiwango cha lami ingekuwa rahisi sana kusafirisha chakula hicho. Hivi sasa ni lazima upite Morogoro ndipo urudi Dodoma. Hii ni mifano michache juu ya namna tusivyotambua nini tunatakiwa kufanya na kwa wakati gani.

Mkuu Mpoki,

Ulichochambua hapa ndivyo serikali yoyote makini inatarajiwa kufanya, lakini sio kwa serikali kama yetu hapa. Mifano zaidi ni barabara ya Tunduma- Mpanda, ambayo inaunganisha mkioa wa Mbeya, Rukwa na Kigoma ambayo uchumi wake katika kilimo ungechangia pato la taifa katika kiwango ambacho hakijawahi tokea tangu tupate uhuru.

Rukwa wanashindwa kuzalisha zaidi kwa sababu wanashindwa kusafirisha mazao kutokana na barabara mbovu, na viongozi wetu hawauoni umuhimu wa barabara hiyo bali kupanua ipitayo kwa Mkuu wa Kaya.

Kiwanja cha ndege cha Songwe Mbeya ni mfano mwingine, ujenzi wake ulianza kuzungumziwa tangu miaka ya 70 lakini ni katika kipindi cha Mramba akiwa RC Mbeya ndipo alipoanza kukiuza kwa wahisani na Prof Mwandosya alipoteuliwa kuongoza Wizara ya Mawasiliano moja ya ujumbe alompa ni kuhakikisha kiwanja hicho kinajengwa kwa maslahi ya taifa.

Mchango wa kiuchumi wa uwanja wa Songwe ni zaidi ya Arusha na Kilimanjaro, Mbeya ni lango kuelekea Kusini, kwa miaka kadhaa mataifa ya Marekani, Ulaya na Asia wamevutiwa na location ya Mbeya kibiashara lakini kikwazo ni uwanja wa ndege.

Tatizo la viongozi wetu vipaumbele vyao ni kwenye matanuzi zaidi kuliko uzalishaji.

Mfano mwingine wa jinsi viongozi wetu wanavyoshindwa kubaini vipaumbele vyetu ni ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, hivi kuna ulazima gani wa kujenga bandari kubwa Bagamoyo wakati zile zingine zilizopo Mtwara na Tanga hazitumiki kikamilifu na wala hazijaboreshwa!

Huyu ni JK na wala sio Kawambwa!
 
Wana JF, mbunge wa Nzega leo ametoa kauli kali pale aliposema kuwa serikali inatumia pesa bila idhini ya bunge

Katoa mifano kuwa barabara ya Chalinze serikali imetumia fedha bila ruhusa ya bunge na kuwaambia mawaziri watalaaniwa na kama hawajui kifo waangalie makaburi.

Wanajamvi kuna yeyote mwenye updates juu ya suala hili?
Jana six alitoa mwongozo kwa kuipa serikali notes ya saa 24 itoe maelezo ya kina kuhusiana na tuhuma hizo za kutumia fedha kabla hazijaidhinishwa na bunge.Kama kuna yeyote amefanikiwa kupata update atujulishe tafadhali.
 
Back
Top Bottom