hii ya kutumia mgongo wa donors ni kuficha uchafu au ukweli., donors huwa anaombwa kufadhili barabara kufuatana na priority zako, sasa ikiwa mimi ninatoka mtera na labda ni waziri wa fedha au wa miundo mbinu , basi nitampa somo donor kumuonyesha umuhimu wa hiyo barabara, basi akiridhia ndio hivyo tena yanakuja ya wengine why not this road or that road. tunachotakiwa ni ile tume ya uchumi, kuwa inapitia projects zote za nchi na kupanga priority zetu kwama ikitokea fedha za donor ama za ndani basi mradi huu ndio wa kuanza then huu etc etc.Sijui Serikali itamjibu namna gani Mheshiwa Spika Sitta ili Mhe. Selelii aridhike.
Lakini sisi Watanzania ni vema tukatambua kuwa ni omba omba wa kutupwa! Kama Denmark imetupa fedha baada ya kupokea ombi letu na kuona tuna shida ya barabara ya Chalinze-Segera, na kwamba ktk Bunge lake huko Denmark, fedha hizo ni lazima zitumike au ziwe "committed" kabla ya June, 2009, basi ni lazima sisi tukubali, hata kama wakina Selelii wangetaka kupitisha "makubaliano" yao. A beggar cannot choose!!! And above all, this is only a question of timing, not a question of where the grant from the donor will go.
By being so beggarly, we as a country have compromised our sovereignty and independence in deciding on so many things that take place in this land. The solution is not to play delaying tactics, but moving positively fast forward with projects which can facilitate genuine development for all of us.
Alichosema Seleli ni kweli tupu na ni mfano mzuri wa kongozi ambaye anaguswa na masuala ya jamii. Yupo pia Siraju Kaboyonga. Nimekuwa nikimsikiliza kwa makini sana kuhusu namna anavyochambua masuala ya msingi ya kiuchumi na kutoa mwongozo. Angesikilizwa tungepata mwelekeo mzuri. wanachosema wabunge hawa ni nini. Katika kipindi hiki cha kuanguka kwa uchumi ambapo uchumi wetu unatarajiwa kushuka kwa asilimia 2 kutoka 7 tulizofikia, kuna kila sababu ya kutafuta njia za msingi za kuhakikisha kuwa hatutetereki zaidi. baadhi ya njia hizi ni kuimarisha miundo mbinu ya ndani ili irahisishe usafirishaji wa bidhaa na kufungua maeneoe zaidi ya kiuchumi ili yachochee ukuaji wa uchumi. Kuunganisha barabara Kuu na kuimarisha usafiri wa reli ingekuwa ni wazo la kwanza. Lakini pia kutazama barabara ambazo zinaingia kwenye maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya utalii. Nitoe mfano mdogo tu. Kutoka Iringa Mjini hadi Ruaha Natioanl Park ni Km. 126 ambazo ni sawa na mwendo wa saa 1:15 kama barabara hiyo ingekuwa ya lami. lakini kwa sasa ili uende huko ni lazima utumie saa 3:00. Hii imefanya Hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa Tanzania kwa vipindi fulani fulani kukosa kabisa watalii wa ndani na nje. Vile vile katika uchumi duni kama wa Tanzania moja ya vitu ambavyo hupandisha gharama ya maisha ni chakula. Hivi sasa mikoa ya Kaskazini na kati kama manyara, arusha, Singida na Dodoma ina matatizo makubwa ya chakula. Lakini kuna chakula cha kutosha katika mikoa ya nyada za juu kusini(Iringa, Mbeya, Ruvuma na Rukwa) hivyo kama barabara ya Iringa - Dodoma ambayo ina Km 240 hivi ingekuwa imetengenezwa kwa kiwango cha lami ingekuwa rahisi sana kusafirisha chakula hicho. Hivi sasa ni lazima upite Morogoro ndipo urudi Dodoma. Hii ni mifano michache juu ya namna tusivyotambua nini tunatakiwa kufanya na kwa wakati gani.
Wana JF, mbunge wa Nzega leo ametoa kauli kali pale aliposema kuwa serikali inatumia pesa bila idhini ya bunge
Katoa mifano kuwa barabara ya Chalinze serikali imetumia fedha bila ruhusa ya bunge na kuwaambia mawaziri watalaaniwa na kama hawajui kifo waangalie makaburi.