Mh. Temba adai Yamoto Band ilisambaratishwa na wenye fedha

Mh. Temba adai Yamoto Band ilisambaratishwa na wenye fedha

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Yamoto-Band.png

Msanii wa Bongo Mh. Temba amedai kuwa chanzo cha kundi la Yamoto Banda kusambaratika ni baada ya watu wenye fedha kuingia kati.

Temba ambaye alikuwa msamamizi na mmoja ya waanzilishi wa kundi hilo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa imekuwa kawaida watu kuona vipaji viking’aa ndipo wanajitokeza kwa mgongo wa kusaidia lakini hawataki kuibua vyao na ndicho kilitokea kwa Yamoto Band.

“Mimi nakupa mfano hawa Yamoto, utaona labda kuna mtu anasimamia msanii fulani, mbona hakumchukua mwanzo wakati hajulikani kabla hatujamkuza na kuwa superstar,” amesema Temba.

“Huyo mtu kama ana uwezo kwanini asingekuwa na vipaji vyake, wewe unaona tayari nuru inang’aa unaenda kuchomoa pale,” ameongeza.

Kundi la Yamoto Band ambalo liliundwa na Aslay, Beka Flavour, Marombosso na Enock Bella kwa sasa kila mmoja anafanya kazi na menejiment yake.

Bongo5
 
Nachowalaumu wametengana kizeeembe mno ilikuwa waachane kwa bifu kali kutukanana matusi kuvuana nguo kwa machozi na damu ingekuwa game changer nzuri sana wamekikosea kizazi chao cha muziki.
 
Warudi tena waungane kwani bado hawajachelewa
 
Ujinga ndio sababu. Manake shule. Mngekuwa na wakili wa kuongoza kampuni kisheria
 
Msanii wa Bongo Mh. Temba amedai kuwa chanzo cha kundi la Yamoto Banda kusambaratika ni baada ya watu wenye fedha kuingia kati.

Temba ambaye alikuwa msamamizi na mmoja ya waanzilishi wa kundi hilo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa imekuwa kawaida watu kuona vipaji viking’aa ndipo wanajitokeza kwa mgongo wa kusaidia lakini hawataki kuibua vyao na ndicho kilitokea kwa Yamoto Band.

“Mimi nakupa mfano hawa Yamoto, utaona labda kuna mtu anasimamia msanii fulani, mbona hakumchukua mwanzo wakati hajulikani kabla hatujamkuza na kuwa superstar,” amesema Temba.

“Huyo mtu kama ana uwezo kwanini asingekuwa na vipaji vyake, wewe unaona tayari nuru inang’aa unaenda kuchomoa pale,” ameongeza.

Kundi la Yamoto Band ambalo liliundwa na Aslay, Beka Flavour, Marombosso na Enock Bella kwa sasa kila mmoja anafanya kazi na menejiment yake.

Bongo5
temba ndezi tuu hajua hata yeye amesambaratika.. hata tmk imesambaratika.. kwa nini ya moto tuu .. chini ya kapeti temba alipiga pesa mingi kupitia hao madogo ndio maana analia lia... ovaaaaaaaaaaaaa..
 
Warudishwe basi kund liwe kama la mwanzo, nawakubali sana yamoto band
 
Nachowalaumu wametengana kizeeembe mno ilikuwa waachane kwa bifu kali kutukanana matusi kuvuana nguo kwa machozi na damu ingekuwa game changer nzuri sana wamekikosea kizazi chao cha muziki.
Duu mkuu umeua.......
 
Mimi nilijua watatengana, watoto washakuwa majukumu yameongezeka, mgao wenyewe si kivile tofauti na wenzao wanaojitegemea, kwa hiyo temba asilete sababu za kitoto mbona wanaume tmk, Wanaume halisi, Watu pori, east cost etc,wote chali.Makundi kidogo yanalipa kama ya kiendeshwa kwa staili ya WEUSI vinginevyo mtalala njaa
 
fella,chambuso, na huyo temba wote sio watu wema wamewanyonya madogo sana we et show moja wanapga mil 10 af et wanapewa lak 1 each one ya matumiz alaf inayobak et inaenda kujenga nyumba zao ambazo mpaka sasa hakuna hata mwenye hat ya nyumba....njoo tabata savanna upate stories kutoka Kwa hao wenyew yamoto tupo nao kitaa hapa kasoro aslay ndo akai huku
 
Mlishatuchosha na siasa zenu kila siku majukwaani mkasahau kazi yenu ya mziki
 
Ukawa utasikia eti bashiti ndo aliwatenganisha ..hahahahahahahahahahahahah hahahahahahhahaahahhaha
 
Nazan ni kwa sababu ya Mkubwa fella kuwadhulumu haki zao hao madogo ( nasikia na zile nyumba sio zao hao yamoto)
 
Bora limesambaratika Tu......vinyimbo vyote vilikua vinafanana beat mpka uimbaji......lkn Sa hv ona wanavoshusha mawe ya maana....Na waliokua wanajificha kwa vivuli vya wenzao wameonekana poa.
 
Back
Top Bottom