Mh. Vicky Kamata CV ...[ Mungu tuokoe]

Status
Not open for further replies.
Huyu ana Division gani toka Form iv hadi chuo bila kupitia FORM VI?.
 
Toka kuzaliwa Septemba 1978 hadi kuanza shule January 1983 ni miaka 4 na miezi mitatu, ndio akaanza darasa la kwanza!
Mwaka wa kuzaliwa utakuwa umesogezwa mbele.
Maybe September 1975, awe ameanza shule akiwa na miaka 7 na miezi mitatu...
Lengo la kusogeza mwaka wa kuzaliwa ni nini vile? Aonekane bado bikra siyo? Ili UVCCM impaishe au? Wanasiasa bana!!! Si mlokole huyu??
 
Pia kumbumbukeni ulaya na marekani unaweza kupata digrii ukiwa na elimu ya darasa la saba, swali la kujiuliza ni ...............je kwa mfumo wa kwetu ni sawa.?
 
Hapo kwenye masters 2008-2008 sijaelewa.

Masters za UK Nyingi ni za Mwaka mmoja Mkuu na Vick ana Diploma ya Nyakahoja mtoa uzi huu hajaina!! Ila hizo publication ni mbili kaziandika mara nne aonekane ni mwandishi mzuri. Sumaye pia amesoma masters wakiwa na diploma tena Havard.
 
Inawezekana mbona Slaa ana PhD bila masters.

Hiyo sio tabu (though sijui kama ni kweli....)

Profesa Wamba Dia Wamba alipokuwa akisubmit thesis ya masters alipewa Phd baada ya kuonekana kuwa kiwango chake si cha kawaida....
 
Sioni tatizo na hiyo CV My take..."ni mpambanaji na maisha, na Masters UK vyuo huwa sio magumashi na its one year..basically 9 months and te rest is research. Hongera Mama.
 
Cha ajabu ni nini nchi za wenzetu kuna vyuo ambavyo kielimu viko kibiashara zaidi,Labda uangalie mfumo wa elimu wa hicho chuo uko je.Inawezekana MSC kwao labda ndio certificate au diploma na siyo kama unavyoifikiria wewe kutokana na mfumo wa elimu wa nchi uliko.
 
Nadhani CV yake ina ulakini vinginevyo mwandishi wa CV hii ambaye ni "Mwenye CV" hakujua alichokuwa anakiandika. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa masomo yake kabla ya MSc yanayomruhusu kuchukia Master Degree in Science wakati background yake siyo ya mchepuo wa Sayansi. Kuna kitu nyuma ya ubao wa CV yake.
 
Jamani unapoandika PUBLICATION kwanza unaanza AUTTHOR NAME, YEAR, TITLE YA PUBLICATION, NAME OF JOURNAL, VOLUME, NUMBER, PAGE

Hivi kweli Viky Kamata hizo zilikuwa publications? mbona hutaji hata journal zilipokuwa submitted?
Halafu Nyakahoja Computer Center hawatoi DIPLOMA Wanatoa Certificate of appreciation/attandance.

Tatizo la CCM kila kitu wamezoea kuchakachua. Hivi mkisema tu UKWELI kuhusu ELIMU zenu mtakufa? au UONGO ndiyo SERA YA CCM. Imagine hata mwaka wa kuzaliwa anadanganya wakati tunajua amezaliwa 1974 na sio 1978? SHAME ON YOU VICKY KAMATA.
 
Nimefurahishwa na Publication zake, yaani Title ni hio hio na imeandikwa kwa mara zaidi ya mbili Duh Kazi ipo
 
Ndugu, hiyo MSc yaweza kuwa katika Uhasibu, mabmo ya fedha nk, si lazima iwe Natural au Applied Sciences zamazoeleweka! Hata pale IFM kuna MSc za aina hiyo.

Mie issue inayonishangaza hapa ni BENKI KUU KUAJIRI Public Relation Officer Mwenye CHETI cha uandishi wa habari bila ya UZOEFU wa kufanya kazi chumba cha habari! Na cheti cha pili cha Customer care alikipata akiwa hapo hapo Benki Kuu, (pengine kwa gharama ya BoT), kilichomwezesha ndugu huyu kuwa PUBLIC RELATION OFFICER 1!

Tena, huyu ndugu alikuwa Katibu wa CCM katika matawi ambapo SHUGHULI za VYAMA zinazuiliwa! Je, kwenye Vyuo vyetu bado kunaMATAWI ya CCM?
My take: hapa haijakaa vema!
 
Hapo kwenye masters 2008-2008 sijaelewa.

Baadhi ya Vyuo Vikuu vya nje unapata Masters kwa mwaka mmoja kwa hiyo sio shida sana, wacha Mdada achape kazi ilimradi anatoa matokeo. Elimu sio vyeti na muda uliotumika kuipata, bali jinsi unavyoitumia kwa manufaa ya Umma.
 
MSc bila first degree? Wewe inakuingia akilini kweli?

Jomba haiingii akilini ........mie nilikuwa namjibu alouluiza Masters kwa mwaka mmoja inawezekana?? Ni kuweka mambo sawa tu jomba....
 
V. Kamata: Investigation of Differentiation in University's MBA Programme - A Case Study of Southampton Solet University, UK.2009
V. Kamata: The Impact of Microfinance Scheme in Boasting Women Income - A Case Study of Pride Tanzania, SAUT, Mwanza2005

Hizo publications mbona ni aina mbili tu zinafana kila kitu mwaka na heading
 
Reactions: FJM
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…