Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,153
- 3,800
Awali ya yote, niipongeze TAKUKURU kwa namna wanavyoshughulikia wezi wa fedha na mali za vyama vya ushirika. Nimeona kule Kusini hasa zao la Korosho, wezi wakiamriwa kurejesha mamilioni ya fedha, Tabora nako nimeona.
Kwa Mikoa ya Shinyanga na Mwanza, kuna Vyama viwili vya SHIRECU (Shinyanga) na NCU( Mwanza), ambavyo vilijihusisha na ununuzi wa mazao hasa pamba miaka ya nyuma. Siyo jambo la kificho,ukweli ni kuwa vyama hivi vilifilisika kwa sababu ya wizi.
Kulikuwa na viongozi ambao baadhi wapo hadi leo walivifanya kama vile ni mali za familia zao na ndugu zao.
Leo hii, ukipita kwenye Ginneries na vituo vyao utatamani kulia kwa namna mali zilivyotelekezwa huku zikioza bila hata kuhifadhiwa. Ikumbukwe hizi ni mali za wananchi,wakulima.
Kuna tetesi zilikuwepo kuwa,Ofisi ya Waziri Mkuu katika awamu zilizopita ilianza kushughulikia hili jambo japo taarifa kamili haikutolewa.
Mali hizi ni mali za Umma, zinaoza peupe kama hazina mwenyewe. Wahujumu wa hivi vyama ni vyema wapatikane,watendewe haki kama inavyofanyika maeneo mengine.