Mh. Wilfredy M. Lwakatare kujiunga rasmi na JF kesho

Mh. Wilfredy M. Lwakatare kujiunga rasmi na JF kesho

Omutwale

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2008
Posts
1,429
Reaction score
1,047
Wapendwa wana ukumbi, JF
Napenda kuwafikishia salamu za utangulizi juu ya kujiunga rasmi kwa aliyekuwa mbunge wa Bukoba mjini kwa tiketi ya CUF mwaka 2000-2005 hapa jukwaani, JF
Mh. Lwakatare atafanya hivyo kesho mida ya mchana. Kama ilivyo ada na utamaduni tunaoujenga hapa jukwaani, tunaombwa kumkaribisha mgeni huyu mwenye hazina muhimu kwa mustakabali wa siasa za nchi yetu.
Binafsi natanguliza shukrani kwa Mh. Lwakatare kwa kukubali mwaliko huu ili aweze kuzungumza moja kwa moja na Watanzania walio katika majukwaa ya mitandao.
 
We eleza tu kwanba huyo Mhe ataongea na wana JF usiseme ni hazina anaweza akawa hazina kwako na siyo kwa watu wote.
 
Mkuu;

Subira kakaaa . . . asipokuja hiyo kesho je?

Si tumsubiri mwenyewe? Ama?
 
Anakaribishwa,

Awe na kifua tu, kifua cha kuchukua maneno maana hapa kuna ya kila aina kutoka kila sehemu ya demographic ya Watanzania.
 
Anakaribishwa,

Awe na kifua tu, kifua cha kuchukua maneno maana hapa kuna ya kila aina kutoka kila sehemu ya demographic ya Watanzania.

Natumaini alikwisha elezwa hilo. Na nilifurahi kusikia kuwa anawajua hata wale waliojaribu kuingia na majina yao, wakakaribishwa, wakachangia lakini kilipoanza kibano, wakaacha ku-log-in kwa hayo majina. Miongoni mwao ni "Dowans", etc
 
Wapendwa wana ukumbi, JF
Napenda kuwafikishia salamu za utangulizi juu ya kujiunga rasmi kwa aliyekuwa mbunge wa Bukoba mjini kwa tiketi ya CUF mwaka 2000-2005 hapa jukwaani, JF
Mh. Lwakatare atafanya hivyo kesho mida ya mchana...
Aaaaaa.. tunajuaje labda wewe mwenyewe ndio Lwakatare!!!!
 
Tusientertain elitism hapa JF. Kama anataka kujiunga aje hapa na kujitambulisha akishakuwa tayari. Watu tuna shughuli nyingi na muhimu zaidi za kufanya kuliko kujitayarisha kumkaribisha yeye. Kama kakutuma mwambie anajitengezea sifa mbaya mapema, kama umejituma mwenyewe basi usirudie tena tabia ya ushabikishabiki.

JF sio chama cha siasa, JF ni jamvi ambalo walioketi wote wana thamani sawa.
 
Ni vizuri anapoingia JF kwa jina lake lakini asije akakimbia kama Zitto alivyofanya mambo yatakapomgeukia, maana hapa haonewi aibu mtu.
 
Ni vizuri anapoingia JF kwa jina lake lakini asije akakimbia kama Zitto alivyofanya mambo yatakapomgeukia, maana hapa haonewi aibu mtu.

Twamkaribisha, twamtisha? Natumai amekuwa akilitizama jamvi letu kitambo kabla ya kuamua kulikalia. Hivyo anajua aina wa wachangiaji waliomo. Mara nyingi Msafiri hujiandaa.Karibu Lwakatare. Kukaa au kuondoka jamvini hiari yako, uhuru wako.
 
Natumaini alikwisha elezwa hilo. Na nilifurahi kusikia kuwa anawajua hata wale waliojaribu kuingia na majina yao, wakakaribishwa, wakachangia lakini kilipoanza kibano, wakaacha ku-log-in kwa hayo majina. Miongoni mwao ni "Dowans", etc

Ni vizuri anapoingia JF kwa jina lake lakini asije akakimbia kama Zitto alivyofanya mambo yatakapomgeukia, maana hapa haonewi aibu mtu.

Sasa wakuu nyie tafsiri yenu ya kukimbia ni nini? mbona muheshimiwa tuko nae hapa na juzi tu (12 June 2009) kaposti hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/1966-zitto-kabwe-atangaza-kung-atuka-19.html#post486568 au ndio maji taka yenyewe haya!
 
Aaaaaa.. tunajuaje labda wewe mwenyewe ndio Lwakatare!!!!

Watu kama SteveD ni wataalamu wa kuwajua watu wanaotumia majina bandia au
majina mengi humu ndani. Si rahisi kuzuga ndani ya jamvi hili, utajulikana tu.
 
mzee omutwale umeshavuta za kampeni nini,
sikuona haja kabisa ya jamaa kuanza kutambulishwa ujio wake humu JF, na ameingia baada ya kushawishiwa ili iweje, humu sio sehemu ya kuingia kwa ushawishi,
hata kama alikuwa mbunge na mpiganaji mzuri sio kwamba akiingia humu ndio atakuwa na hoja ambazo azipingiki, aje na hoja na awe tayari mkupingwa kwa hoja
 
Ujumbe wako ataukuta, kuusoma na ataufanyia maamuzi mwenyewe

Omutwale, sidhani kama ulikuwa na sababu ya kuja na matarumbeta kwa new member kama tuko wenye harusi pale kipleft cha Impala hotel!!!

Nina wasiwasi na hizi campaign za chinichini hapa.... tutasikia mpaka wabunge wote wanaingia na entourage humu ...akija apige hodi na si kupigiwa hodi

Waitu anyway!!!
 
Hahaaa umenikumbusha jamaa fulani alienda soma majuu kwa myaka miwili, alipo rudi anafika airpoti, akakuta kaandaliwa msafara hadi wa matarumbeta! jamaa alinitonya kwamba alijisikia vibaya hadi shati lililowa jasho ghafla!

Lwakatare karibu, ila huyu aliyeleta matarumbeta mhhh..
 
Wakuu kujipigia matarumbeta inaruhusiwa na hata kujifagilia...Karibu Mh Lwakatare!
 
Mbona muheshimiwa kimya.....Omutwale Vipi muheshimiwa kapatwa na miguu baridi nini??
 
Mbona muheshimiwa kimya.....Omutwale Vipi muheshimiwa kapatwa na miguu baridi nini??

Nina hakika alifika hapa jukwaani jana.

Kwa leo na siku 2-3 zinazokuja natumaini atakuwa busy kujiandaa na safari ya kwenda BK kupata ushauri wa wananchi juu ya nini afanye na nini kifuate.

Wananchi watampa majibu juu ya kwa nini ahame CUF, na wanataka ahamie chama gani.
 
Back
Top Bottom