Mh. Wilfredy M. Lwakatare kujiunga rasmi na JF kesho

Mh. Wilfredy M. Lwakatare kujiunga rasmi na JF kesho

Nina hakika alifika hapa jukwaani jana.

Kwa leo na siku 2-3 zinazokuja natumaini atakuwa busy kujiandaa na safari ya kwenda BK kupata ushauri wa wananchi juu ya nini afanye na nini kifuate.

Wananchi watampa majibu juu ya kwa nini ahame CUF, na wanataka ahamie chama gani.

Mwambie asiende CCM tafadhali...asante sana! we might need him upinzani..
 
Mwambie asiende CCM tafadhali...asante sana! we might need him upinzani..

Kama ukiweza soma Nipashe ya leo au MwanaHalisi ya toleo la sasa (not of 2mrw). Pia unaweza kudadisi kwa waliosikiliza Radio WAPO FM jana saa tano mpaka saba. Huko kote Lwaks amesema anaweza kuhama CUF lazima hawezi kamwe kuhamia CCM.

Kuna minon'gono kuwa CCM wametoa offer ya kumpa jimbo na Kagasheki ku-step down kama alivyotangaza. Lakini pia leo hii ujumbe wa CUF taifa umetuma wajumbe Ibwera kwa Baba yake Lwaks kumwomba amshawishi mwanae asitishe mpango wowote wa kuhama chama. Usinihoji zaidi juu ya logic/busara ya CUF kupitia kwa Baba mtu maana mie ni messenger, mimi tu kukufikishia ujumbe.
 
Omutwale

Asante sana nimekusoma mfikishie salaam kwa niaba ya wanaJF...tunamkatakia kila laheri, asiwe cheap kuhongwa jimbo ama chochote...bahati mbaya huku New Zealand sina access ya hayo magazeti, JF hunipa kila kitu...kama Babu akata Kusema atakumbuka kupaste hapa!
 
Wapendwa wana ukumbi, JF
Napenda kuwafikishia salamu za utangulizi juu ya kujiunga rasmi kwa aliyekuwa mbunge wa Bukoba mjini kwa tiketi ya CUF mwaka 2000-2005 hapa jukwaani, JF
Mh. Lwakatare atafanya hivyo kesho mida ya mchana. Kama ilivyo ada na utamaduni tunaoujenga hapa jukwaani, tunaombwa kumkaribisha mgeni huyu mwenye hazina muhimu kwa mustakabali wa siasa za nchi yetu.
Binafsi natanguliza shukrani kwa Mh. Lwakatare kwa kukubali mwaliko huu ili aweze kuzungumza moja kwa moja na Watanzania walio katika majukwaa ya mitandao.

Kesho ya jana si ndo hii.....mbona kimya? Ngoja tuwe na subira anyway!.....personally I need him to clarify some issues!
 
Wapendwa wana ukumbi, JF
Napenda kuwafikishia salamu za utangulizi juu ya kujiunga rasmi kwa aliyekuwa mbunge wa Bukoba mjini kwa tiketi ya CUF mwaka 2000-2005 hapa jukwaani, JF
Mh. Lwakatare atafanya hivyo kesho mida ya mchana. Kama ilivyo ada na utamaduni tunaoujenga hapa jukwaani, tunaombwa kumkaribisha mgeni huyu mwenye hazina muhimu kwa mustakabali wa siasa za nchi yetu.
Binafsi natanguliza shukrani kwa Mh. Lwakatare kwa kukubali mwaliko huu ili aweze kuzungumza moja kwa moja na Watanzania walio katika majukwaa ya mitandao.

Omutwale, hii ilikuwa 15/06/2009, Hivi hiyo kesho haijafika, au ulimaanisha siku itakapofika ile siku inayoitwa kesho?.
 
Back
Top Bottom