BilioneaPATIGOO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 12,320
- 11,327
Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa jana jioni alikwenda Genk nchini Ubelgiji nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta.
Zitto amesema kuwa amefurahi kumsalimia na kumjulia hali Samatta huku akieleza kuwa amefurahi kumkuta akiwa mzima wa afya.
Aidha Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa “Nilipata nafasi kumsalimu @samatta77 jana jioni nyumbani kwake Genk. Nimefurahi kuwa anaendelea vizuri na anapambana kuhakikisha anaendelea kukuza nchi yake na yeye mwenyewe. Ana mawazo mazuri Sana ya kuendeleza soka la Tanzania. Mungu atamsaidia Samata wetu Watanzania,”
Pia Mh. Zitto kupitia ukurasa wake wa Twitter amemjibu Yericko Nyerere na baadhi ya watu waliokua wanajiuliza kwamba kwanini Samatta haendi kumjulia hali Mh.Lissu hospitalini, akiwatahadharisha ya kwamba naye pia Samatta ni mgonjwa kwahio yupo katika ratiba ngumu ya mazoezi ya kurudi katika hali yake ya kawaida chini ya uangalizi mkubwa wa daktari wake, kwahio hawezi kwenda kinyume na ratiba hio tofauti na huku kwetu tunavyofanya, kwahio anaomba msimhusishe na mengine kwa wakati huu ambapo yuko katika program na uangalizi maalumu wa afya yake na mazoezi. Aidha amesema kwa wakati na muda wake ambao ataruhusiwa atakwenda kumuona.
Klabu ya KRC Genk ambayo Mbwana Samatta anacheza ni mojawapo ya klabu za mpira tajiri nchini Ubelgiji, ambapo kijana wetu anaweka kibindoni
Milioni 55 kwa mwezi. Tumtakie heri arejee dimbani.