Mhadhiri CBE: Benki ziwafuate wananchi vijijini

Mhadhiri CBE: Benki ziwafuate wananchi vijijini

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Mhadhiri wa chuo cha Biashara CBE, Dkt Dickson Pastory amezitaka benki hapa nchini kuongeza ubunifu wa kuongeza mapato yake kwa kutazama vyanzo vingine ikiwemo kuwafikia wananchi waliopo vijijini.

Amesema benki nyingi hutegemea mapato yatokanayo na utoaji wa mikopo hivyo riba zinaposhuka nazo mapato hushuka hivyo badala ya zenyewe kuongeza gharama za miamala kitu ambacho kitaondoa hamasa ya wananchi kutotumia benki ni vyema wakatazama fursa ya wananchi walio wengi vijijini.

Amesisitiza uamuzi wa BoT kushusha riba ni mzuri kwani umelenga kufikia maono ya Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ya wananchi wanyonge kupata mikopo kwa masharti nafuu ikiwemo riba ili waweze kushiriki katika shughuli za uzalishaji kama vile kilimo au ufugaji wa kisasa au umiliki wa viwanda vidogo vidogo na vya kati na hivyo kuinua uchumi wa nchi yetu na kutoa ajira nyingi zaidi.

IMG-20190207-WA0034.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilihisi tu huyu Dkt atakuwa wa CBE
 
Back
Top Bottom