Mhadhiri UDOM aliyetaka rushwa ya ngono kwa mwanafunzi afunguliwa shtaka la uhujumu uchumi

Mhadhiri UDOM aliyetaka rushwa ya ngono kwa mwanafunzi afunguliwa shtaka la uhujumu uchumi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma inatarajia kumfikisha mahakamani Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Jacob Nyangusi (43) na kufunguliwa shauri la uhujumu uchumi kwa kosa la kutaka rushwa ya ngono kinyume cha sheria ya kuzuia na Kupambana na rushwa namba 11/2007.

Mkuu wa Takukuru Dodoma, Sosthenes Kibwengo, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema watamfikisha mahakamani leo jijini Dodoma.

Alisema majira ya saa 3 usiku Oktoba 3, 2018 Takukuru ilimkamata Nyangusi akiwa nyumbani kwake eneo la nyumba mia tatu jijini Dodoma muda mfupi kabla hajatekeleza nia ovu ya kufanya ngono na aliyekuwa mwanafunzi wake wa mwaka wa kwanza wa shahada ya Sanaa katika Jiografia na Mazingira.

Alisema awali alipokea taarifa kuwa mtuhumiwa alimtaka mwanafunzi wake kingono kama sharti la kumsaidia ili aweze kufanya mitihani ya marudio na kumuwezesha kufauli katika somo lake.

“Ndipo tukaweka mtego kumkamata baada ya uchunguzi kukamilika na Ofisi ya Mashtaka kuridhia kwa mujibu wa sheria ndipo mtuhumiwa anafikishwa mahakamani,” alisemaKibwengo

===
Pia soma

Mhadhiri UDOM ashikiliwa na Vyombo vya Dola kwa tuhuma ya kutaka rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wa kike
 
Tatizo wahadhiri wengi walikuwa soma soma enzi za shule.. hawana uzoefu wa kutongoza wanawake na hawajui wanawake wanataka kusikia nini ili wakupe mzigo...

Ndio maana vijana wa kitaa wanajilia warembo bila shida..

Inabidi ianzishe twisheni ya kutongoza..
Wengi wamezaliwa shamba wamepata first class wameajiliwa ushamba mwingi wa mademu
 
Wameamua kumtoa mbuzi wa kafara ...

Kitendo alicho kifanya huyo muomba rushwa ya ngono sio cha kibinaadamu mwenye utu anavyo paswa kuwa ..but trust me mpaka wame amua kumkamata kwa hizo tuhuma itakuwa yeye na viongozi wenzake wa hapo chuo walikuwa na migongano yao binafsi ya kimaslahi ...so wameamua wa mtoe kafara kimtindo huo
 
LOL... Amehujumu uchumi wa nchi, siyo? Uchumi wa nchi umekaa hapo katikati, siyo? Sitetei alicholifanya lakini jamani hii sheria ya uhujumu uchumi siyo ya kukomoana kweli?
Uhujumi uchumi cause huyo mwanafunzi ni rasilimali ya serikali .. So ukiitendea ndivyo sivyo rasilimali ya taifa inaachaje kuwa sio uhujumu uchumi!??
 
Mbunye imemponza kijinga sana ila pale UDOM kuna ma lecture maninga sana kwenye Mbunye natamani niyataje ila ngoja nikaushe
 
Back
Top Bottom