Ferruccio Lamborghini
JF-Expert Member
- Apr 15, 2020
- 1,667
- 2,595
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, alifikishwa mahakamani jana. Ni matokeo ya tuhuma zinazomuandama kwa muda mrefu sasa.
Yameshasemwa na yanaendelea kusemwa mengi. Hisia ni tofauti kuhusu yanayomtokea Sabaya. Kila mtu anataka aseme kitu. Nami nimeshaulizwa kwa nini sisemi chochote. Ngoja basi nitoe neno. Nitachukua muktadha maalum, bila kuingilia uhuru wa mahakama.
Tuhuma za Sabaya ni nyingi, zinaogopesha. Zinashangaza kupita kiasi. Zinahitaji akili ya juu mno kuzichambua. Ukizichukua tuhuma za Sabaya na kuziweka kwenye kapu la uhalifu sawa na uhalifu mwingine, hilo ni kosa kubwa.
Tafakari, Sabaya ni binadamu. Kila binadamu ana ubinadamu, vinginevyo kuwe na shida kwenye ubinadamu wake.
Tafakari zaidi, Sabaya akateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya. Kazi ya kutumikia wananchi. Binadamu wenzake. Kila binadamu anafamu wito wa ubinadamu ni kuwatendea haki binadamu wenzake. Vinginevyo ubinadamu wake uwe na upungufu.
Inafahamika, kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa kiongozi ni zawadi kubwa mno. Kuilipa hiyo zawadi si kufanya chochote isipokuwa kuwatumikia watu kwa upendo na uadilifu.
Sabaya akiwa mkuu wa wilaya, akawa anatuhumiwa kupora mali za watu, kuonea anaowaongoza. Kulazimisha mapenzi kwa wanawake na hata kubaka. Hizo tuhuma ukizisikia, kama una kichwa kizuri lazima kwa asilimia 50 utadhani anasingiziwa.
Ni kwa sababu, mtu mwenye akili timamu hawezi kufanya hata robo ya yale anayotuhumiwa nayo Sabaya.
Mtu mzima anawezaje kuteka wake za watu na kulazimisha mapenzi? Anaingiaje kwenye hoteli na kulazimisha aoneshwe chumba cha mteja mwanamke, ili iweje? Anawezaje kulazimisha wafanyabiashara wampe pesa bila kufanyia kazi? Anawezaje kuteka watu na kuwatesa? Anafyatuaje risasi hovyo? Mtu mwenye akili timamu kweli?
Kwa kiongozi, vitendo vyote hivyo kwa sehemu kubwa vinanajisi uongozi. Je, Sabaya kama mtu timamu, hakutambua uongozi ni upendeleo na ulinzi wake ni uadilifu?
Ndio maana nikasema, tuhuma za Sabaya kwa asilimia kubwa hukaribisha hisia kwamba anasingiziwa. Maana mtu mwenye akili timamu hawezi kufanya japo robo ya vitendo anavyotuhumiwa navyo Sabaya.
Sasa, hata baada ya kufikishwa mahamani, lipo eneo la kulisemea. Ni namna ya kuingia ndani zaidi kwenye tuhuma zake.
Nimeshasema, ni kosa kubwa kuziweka tuhuma za Sabaya katika kapu moja la uhalifu, sawa na uhalifu mwingine.
Kama yote ambayo Sabaya anatuhumiwa nayo ni kweli kayatenda, basi uhalifu mkubwa upo kwenye namna ubongo wake unavyofanya kazi. Inawezekana haupokei na kutafsiri mambo kama binadamu wa kawaida.
Kama ndivyo, hata sasa akiwa mahabusu, inawezekana akawa haelewi kwa nini amekamatwa, kwani yote aliyokuwa anafanya (ikiwa ni kweli), yeye anaona alikuwa sahihi. Tena, si ajabu anajiona anasingiziwa.
Watu wenye namna ya kipekee katika kupokea na kutafsiri mambo kijamii huitwa "psychopath". Ni tafsiri sawa na mgonjwa wa akili. Kwa kawaida psychopath huwa wana matatizo ya afya ya akili.
Kama kutakuwa na dhamira ya kumtendea haki Sabaya, basi itabidi kumpima afya ya akili. Maana, kama kweli alitenda yote anatuhumiwa nayo, maana yake atakuwa psychopath. Mtu timamu asingethubutu kufanya hata moja ya 10 ya anayotuhumiwa kufanya.
Binafsi ningetamani, kabla hata hajafikishwa mahakamani, wakati wa kumhoji Sabaya ili kukamilisha taarifa za mashitaka dhidi yake, kungekuwa na wataalamu wa afya ya akili katika mahojiano.
Hapa sipendekezi Sabaya apewe msamaha kama tuhuma dhidi yake zina ukweli, la, haki itendeke. Wahalifu wenye matatizo katika afya ya akili hufungwa, ila kuna namna ya kuwasaidia kipindi wanatumikia adhabu zao.
Kinachonishawishi kuona ulazima wa Sabaya kupimwa afya ya akili ni kwa sababu nataka kujua ubongo wake ulikuwa unawaza nini alipokuwa akitenda uhalifu alioutenda. Hii ni kama kweli alitenda.
Je, ubongo wake ulikuwa unawaza nini? Kwamba yeye ni mkubwa sana kwa hiyo angetenda chochote kwa watu bila lolote kumrudia? Alikuwa anaamini ni haki yake kutendea watu alivyowatendea? Alichokuwa anakitafuta ni kipi hasa? Aliwahi kufikiria kwamba kila tendo lake baya lingemrudia? Ni ni kama kweli tuhuma dhidi yake ni za kweli.
Hata sasa, je, anachukuliaje mashitaka dhidi yake? Anahisi anaonewa? Anachukulia kesi dhidi yake ni ya kisiasa? Anajua mahali alipo? Au kuna mtu alikuwa anamtuma, anampa kiburi, sasa hivi hayupo? Kuna ulazima mkubwa wa kumpima afya ya akili. Itasaidia pakubwa.
Mtazamo wangu katika tuhuma za Sabaya upo hapa, ama anasingiziwa, na kama hasingiziwi, basi kichwani sio mzima. Ni psychopath.
Credit: Luqman Maloto