mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,517
- 6,074
Hapa ndipo watanzania tumefika. Mahubiri ya haki si kwa mtanzania mmoja, bali kwa kila mtanzania, hii mihimili mitatu hii inayoendeshwa na mtu mmoja madhara yake ni makubwa sana
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwalyambi amesema kuwa imani yake ni kuwa mtu pekee anayeweza kumsaidia kwa sasa ni Rais Samia baada ya madai yake kugonga mwamba mahakamani
Aidha, akifafanua kuhusu changamoto iliyomfanya kumuangukia Rais Samia, Mwalyambi amesema "miaka 13 iliyopita alisaini mkataba na serikali kwa ajili ya ujenzi wa barabara Mkoani Rukwa na kudai kuwa alifanya kazi na kuukamilisha mradi huo
Ameendelea kueleza kuwa wakati akiendelea na kazi ulitokea mvutano na kuambiwa kuwa alikuwa anadaiwa na serikali asilimia 20 ya kazi ambayo hajaikamilisha, ambapo yeye alisema "kama asilimia 20 mnasema haijakamilika basi naomba mnilipe asilimia 80 ya kazi niliyoifanya"
Mwalyambi amedai kuwa baada ya mvutano usiokuwa na mafanikio aliamua kupeleka kesi Mahakamani ambapo Hakimu alifanya maamuzi na kusema kuwa "kwenye mradi huo wewe unadaiwa Tsh Milioni 29, lakini wewe unaidai Tsh Milioni 800 hivyo basi natoa maamuzi mmalizane wewe usilipe hiyo Milioni 29 unayodaiwa lakini pia Usilipwe hiyo Milioni 800 unayodai"
Kutokana na Maamuzi hayo Mwalyambi aliamua kukata rufaa ya kesi hiyo lakini juhudi zake hazikuzaa matunda na baadae aliamua kuiondoa kesi hiyo mahakamani baada ya kufuatwa na watu wasiojulikana ambao walipa siku 2 za kuondoa kesi mahakama na wakamwambia akikaidi maagizo hayo watamuua, hivyo kutokana na shinikizo la watu hao alikubali kuondoa kesi mahakamani ili anusuru maisha yake.
Ameongeza kuwa kutokana na vitisho kutoka kwa watu wenye mamlaka aliamua kukimbilia nchini Kenya kwenye kambi ya wakimbizi inayoitwa ‘Capital West’ ambapo akiwa huko alishauriwa arudi nchini na kuendelea kujaribu kuitafuta haki yake.
Pia soma: Mzee aliyedai kudhurumiwa na TANROADS asema "Maisha yangu yako hatarini, napata vitisho, nisaidieni"
==================================
Mmiliki wa Kampuni ya Ruhama 333, Mhandisi Owden Mwalyambi amemuangukia Rais Samia Suluhu Hassan kumuomba msaada ili aweze kulipwa malipo yake, kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mia nane (Tsh 800,000,000/=) anayodai kufanyia kazi mradi wa serikali mkoani Rukwa bila kulipwa.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwalyambi amesema kuwa imani yake ni kuwa mtu pekee anayeweza kumsaidia kwa sasa ni Rais Samia baada ya madai yake kugonga mwamba mahakamani