Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Wakuu,
Huyu baba nlikuwa simpendi jamaniiiiii, bora wamekiondoa, kila kitu cha digitali kwake ni kama haramu, mbwa kabisa!!
YAH: UTEUZI NA KUPANGIWA KITUO BALOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na kumpangia kituo Balozi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na kupangiwa kituo Balozi ni kama ifuatavyo:-
(i) Mhandisi Peter Phillip Mwasalyanda ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Mwasalyanda alikuwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), anachukua nafasi ya Dkt. Jabiri Kuwe Bakari ambaye amemaliza muda wake;
(ii) Dkt. Jabiri Kuwe Bakari ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Dkt. Bakari anachukua nafasi ya Bw. Salim Ramadhani Msangi ambaye atapangiwa majukumu mengine;
(iii) Mhe. Angela Charles Kizigha ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Jamii; na
(iv) Balozi Mobhare Holmes Matinyi amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria.