Tumeona picha ya Rais Kikwete kumfariji muandishi huyo pamoja na kutowa agizo washughulikiwe waliohusika na kitendo hicho ingawaje hakutoa muda fulani kama alivyotowa kwa wale waliouliwa kwa kutuhumiwa ni majambazi,nakumbuka Rais Kikwete alitoa muda wa wiki sita, wametafutwa na kupatikana wapelekwe kwenye vyombo vya sheria,tokea siku ile mpaka leo kimya hakuna kinacho sikika
baada ya Abdalla Zombe kufikishwa mahakani siku mbili tatu kiasi cha kuzibwa macho raia.
Haya tuje kwa Ditopile halkadhalika mambo yalikuwa moto moto wananchi kutia matumaino sheria itachukuwa mkondo wake,lakini wapi zilikuwa ni kelele za mlango leo Ditopile niliwahi kusoma kuwa yuko nje na anafanya biashara zake.Kusudio ni kusema kuwa kama wanavyosema wenyewe "CCM INA WENYEWE" na wenyewe ndio hao watu fulani, pameulizwa muandishi wa habari kosa lake ni nini?
Nami nauliza Marehemu Amina Chifupa kosa lake ni nini? lilikuwa nini?
Tuje kwa Jeneral Ulimwengu, Ali Mohamed Nabwa, ni nini kosa lao hata kufikia kunyang'anywa uraia wao, huyo Mwinyi Sadalla amesha pandishwa kizimbani ni nini kosa lake,ambaye inasemekana ni mtu wao CCM-SMZ.