Mhe. Kwagilwa Nhamanilo - Mama Samia Suluhu Hassan Apewe Maua Yake

Mhe. Kwagilwa Nhamanilo - Mama Samia Suluhu Hassan Apewe Maua Yake

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. KWAGILWA NHAMANILO ASEMA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN APEWE MAUA YAKE

"Niendelee kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Amir Jeshi Mkuu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa uongozi wake bora na thabiti wenye mafanikio makubwa hususani katika kuleta mageuzi ya kiuchumi pamoja na kuimarisha mageuzi ya kisiasa nchini na mahusiano ya kikanda na Kimataifa katika kipindi kifupi cha Miaka Miwili ya uongozi wake hakika Mama apewe Maua yake" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Naungana na Waziri wa Fedha na Mipango kwa kusema Mama apewe Maua yake kwasababu mwaka 2022 tulikuwa na bajeti ya Shilingi Trilioni 41.48. Bajeti ya mwaka 2023 tunayoenda kuipitisha ni ya Shilingi Trilioni 44.39, hili ni ongezeko la Shilingi Trilioni 3 (7%) - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Miaka 2 iliyopita tulishauri hapa kwamba nchi yetu ifanyiwe Credit Rating, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ikafanya hivyo. Sasa nchi yetu iko Rated na makampuni mawili Makubwa Duniani. Makampuni tuliowapa kazi ya kutusimamia na kutushauri kwenye mambo ya fedha wametoa taarifa yao ambayo imedhihirisha kwamba Mama apewe Maua yake" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Kwenye bajeti yetu mapato yameongezeka. Pia, hatua zote za kikodi tulizochukua zinatufanya Tanzania tuendelee kuwa nchi inayokopesheka na tutaendelea kuaminika kwenye masoko makubwa ya kifedha Duniani. Makampuni mkubwa wanastaajabu sana pamoja na kipindi kigumu ambacho Dunia inapitia kiuchumi" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Higher Spending for Ongoing Infrastructure Projects. Kampuni zinashangaa inawezekanaje Tanzania inaongeza bajeti na inaenda kuongeza makusanyo ilihali inapeleka fedha nyingi sana kwenye miradi mikubwa ambayo kwa Ukanda wetu wa Afrika hasa Kusini mwa Afrika hakuna miradi kama hiyo" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Mradi wa Reli ya SGR unajumuisha ununuzi wa vichwa na mabehewa. Nashauri tutafute vichwa na mabehewa kwa safari moja ya Serikali halafu tuwaachie sekta binafsi ifanye eneo la vichwa na mabehewa" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere zinakwenda Trilioni. Ujenzi wa daraja la Busisi, Skimu za Umwagiliaji, Ujenzi miundombinu Mji wa Serikali Mtumba Dodoma" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Wanaendelea wanasema inawezekanaje watanzania wanayafanya haya wanapeleka miradi ya barabara. Tumesaini Mikataba ya barabara mingi sana. Wanashangaa kuona miradi ya Maendeleo ya kijamii" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Hakuna mahali Tanzania hapajengwi Kituo cha Afya, Hospitali, Shule, Umeme. Hakika Mama apewe Maua yake" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini
 

Attachments

  • maxresdefaultvbnhj.jpg
    maxresdefaultvbnhj.jpg
    69.4 KB · Views: 6
Kwa misifa hatujambo na tunajitahidi haswa

Nasubiri siku wakisimama wakasema tumeacha wizi, hapo kwenye rated tutakuwa mbali zaidi
 
Hiyo bajeti ya ongezeko la 7% mnayo? Mtaweza ku disburse hiyo pesa au kushangilia ujinga? (Increase vs disbursement)?
 
Back
Top Bottom