Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,053
- 2,207
hizi za lema ndio porojo na fujo tunataka katiba sio maneno..tunataka katiba mpya lakini uongo wa kudai katiba kufanya fujo....kama munayo munayo pendekeza itoeni hapa tuijadili...kusema tu tunataka katiba mpya bila kusema unataka nini ndani ya hio katiba ni uenda wazimu....katiba sio msahafu au injili ambayo binaadam wameteremshiwa na allah,,,,ni sheria ya nchi inayotungwa na binaadamu so hatutaki porojo la katiba bila kusema nini tunataka...wekeni hapa nini kinatakiwa tukijadili....sio porojo
wewe unaishi Tz kweli?sababu ya kwanza ya kudai katiba mpya ni kwa sababu hii iliyopo haikushirikisha wanananchi.
Kuna mambo mengi specific mfano muundo wa muungano,NEC huru,Wabunge wa kuteuliwa,ukubwa wa cabinet,vyombo vya umma kuwajibika kwa serikali na sio chama tawala.....nikiendelea kutaja naweza kujaza server bure!
Alichokitaka lema ni kwamba serikali iwe wazi,iseme kwamba inaleta mchakato wa katiba mpya na sio kuibuka na porojo na misemo tata kama 'kuhuisha' n.k
tatizo lenu mkiambiwa ukweli mnasingizia fujo.