Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Miongoni mwa udhaifu mkubwa kabisa wa mainstream media zetu zote za Tanzania, si TV, Redio, wala Magazeti, hatuna kitu kinachoitwa "News Analysis", yaani uchambuzi wa habari, viongozi wetu wakihutubia, media inaripoti wamesema nini, the story ends there! Hakuna any news analysis ya kuchambua alichokisema kiongozi huyo wala what does it mean, the impact ya kilichozungumzwa, na the consequences.
Kazi za media zetu ni kuripoti tu kama kasuku. Angalau sisi JF, ndio angalau tunafanya uchambuzi, alichofanya Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, ni a very good piece of news analysis ya hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa Ikulu ya Chato na update ya Corona iliyotolewa na Waziri Mkuu.
Mnyonge, mnyongeni, haki yake mpeni. Tangu kuingia kwa janga hili la Corona, sio tu hakuna kiongozi yoyote amewahi kuizungumzia Corona vizuri na kwa ufasaha kama Mhe. Freeman Mbowe, bali pia tangu nimemfahamu Mbowe na kumsikia, hajawahi kuzungumza vizuri hivi hata mara moja. Freeman, you are the best, hongera sana!
Ila sehemu moja tu ndiyo Mbowe ameharibu, kwenye idadi ya vifo vya Corona. Serikali ilishatoa waraka kuwa wasemaji wa update ya Corona kwa Tanzania ni watu 5 tu. Rais, Makamo, Waziri Mkuu na Waziri wa Afya -- then update ya Corona itatolewa na serikali tu. Sasa kama Waziri Mkuu kasema vifo vya Corona ni 16 tu, then huu ndiyo ukweli. Tanzania watu waliokufa kwa Corona mpaka sasa ninapoandika hapa, ni watu 16 tu na huu ndio ukweli wenyewe.
Kitendo cha kumuita Waziri Mkuu wa JMT kuwa ni muongo na serikali inaficha data za vifo vya Corona, huu ni uongo na uchochezi.
Kati ya Mhe. Mbowe na Waziri Mkuu wa JMT, nani ni mkweli na nani ni muongo? Watanzania wamwamini nani kati ya Waziri Mkuu wa JMT na Waziri Mkuu kivuli?
Kama serikali imesema vifo ni 16 tu, then vifo ni 16, hata kama umeshuhudia watu 100 wakizikwa na serikali kwa mazishi ya kuhudhuriwa na watu kumi tu. Ukweli wa idadi ya vifo vya Corona ni vifo 16 tu kwasababu sio kila anayekufa amekufa kwa Corona. Hata kama hao wengine wote nao pia walionesha dalili kama za Corona, mamlaka pekee inayojua mgonjwa kafa na nini, ni madaktari tu. Na kwenye case ya Corona, waliokufa kwa Corona ni watu 16 tu, hawa wengine wote wanaokufa kwa matatizo ya kupumua, hayo ni matatizo yao tu, na pia wagonjwa wa magonjwa mengine pia wanaendelea kufa, ili kuzuia mikusanyiko katika misiba, serikali imeamua kuwakinga watu wake kwa kujitolea kuwasaidia Watanzania wengine wote kwa upendo kwa kuwazikia ndugu na wapendwa wao.
Hivyo Mhe. Mbowe, asante kwa kuongea vizuri ila uache uongo na uchochezi kuisingizia serikali yetu inaficha kitu, serikali yetu ni wakweli, hawafichi kitu, waliokufa kwa Corona mpaka sasa ni hao 16 tu, na huo ndio ukweli wetu, tena ni afadhali ya sisi tumetangaza ukweli wa wote waliokufa kwa Corona nchini kwetu ni hao 16 tu; je, ungekuwa unaishi Rwanda na Uganda, kule hakuna hata mmoja aliyekufa, ungesemaje?
Watanzania wenzangu ambao ni wazalendo, naombeni tuendelee kuiaminia serikali yetu kuwa inasema ukweli wote kuhusu Corona, tusiwasikilize, waongo, wazushi, wachochezi na wachonganishi wanaotaka kuichonganisha serikali na wananchi, kwa kuwadanganya kila anayekufa, amekufa kwa Corona, japo ni kweli vifo vya ghafla vimeongezeka, ila siyo vifo vyote ni Corona. Vifo vingine ni magonjwa mengine ukiwemo matatizo ya kupumua.
Tena katika kusisitiza uzalendo, nitawaomba kuanzia saa 1:30 asubuhi nitakuwa live Star TV mgeni wangu akiwa ni Deodatus Balile wa gazeti la Jamhuri, tutasisitiza uzalendo na kuiaminia serikali na sio kuwaaminia wazushi.
Paskali