Mkuu
Beatrice Kamugisha , ili mtu kutoa hoja za majumuisho, ni lazima zitanguliwe na hoja za msingi, jee hoja za msingi ni zipi ili ndio tuje kwenye majumuisho?, kama hoja tuu za msingi hazipo, hayo majumuisho yatoke wapi?.
P
Mkuu mimi ni mwana ccm ,Kuna mambo yatupasa kuyabadili tukishinda na tutashinda hasa mtazamo juu ya wananchi na Itikadi yetu
Twende mbele turudi nyuma Tundu lissu ametuzidi kwa hoja na ameelimisha wananchi sana juu ya haki zao na mamlaka yao juu ya Taifa hili
Hoja ya biashara na sekta binafsi kuwa hoe hae wewe mwenyewe una maisha ya kuunga unga awamu hii kama mwanahabari na ulikuja kulalamika hapa,Leo unataka kujitoa ufahamu eti hoja zipi
Pili,Hoja ya bima ya afya kwa kila raia kwani ugonjwa haupigi hodi
Hoja ya maendeleo ya watu yaani mzunguko wa pesa kiujumla una madhara gani kwa jamii husika,Je mambo ya vitu kama ndege vinamgusa vipi mwananchi wa chini kabisa
Mambo ya ajira ,Uhuru wa habari
Sheria ambazo zinazuia uhuru wa kupata takwimu au habari yote hayo yameongelewa
Yafuatayo ccm lazima iyafanye
Kujenga umoja wa vyama vyote na upendo
Kurudisha uchumi mikononi mwa raia ,serikali ibaki kama msimamizi
Kukubali hoja mbadala na kuzijibu kwa ustaarabu
Kupunguza hasira ,panic na dharau ukipewa mamlaka,Ni lazima tuone wananchi ndio wametupa heshma ya uongozi
Wewe umelalamika hapa JF leo usijitoe ufahamu,Toa ushauri nini kifanyike tusipate taabu kama uchaguzi huu tena