Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

Lissu alimnyanyasaga sana Spika Makinda, kwa Spika Ndugai amembananisha.

Pole Tundu Lissu.
P
 
Leo ni Tundu Lissu day, ilikuwa arejee, leo, japo hakurejea, tunamuadhimisha kwa kumtafakari kwa sababu


Leo siku ya tarehe 7/Sept. 2019 ni siku ya kumbukumbu ya miaka miwili toka Mh.Tundu Lisu aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Mpaka leo bado wasiojulikana hawa bado hawatajulikana na uchunguzi mkubwa, makini na mkali wa Jeshi letu adilifu la polisi, unaendelea kuwabaini wasiojulikana hawa, hivi sasa kuna mashuhuda wawili muhimu sana, wanasubiriwa wao tuu kuhojiwa ndipo taarifa rasmi ya polisi kuhusu maendeleo ya uchunguzi huu ndipo ilatolewa.


Tuvute subra.

Get well soon Mhe. Tundu Lissu and welcome back home.

P
 
Mayalla, wewe na Lissu mnalingana?
Ona aibu mdogo wangu.
No mimi na Lissu, hatulingani, japo tulikuwa shule moja Ilboru, mimi nikiwa A level, Lissu alikuwa O-level hivyo kwa Lissu mimi ni Kaka yake, na yeye ni mdogo wangu.
Nimeisha mzungumza sana Lissu humu jf.
Kama hapa, Jee 2020 kuna mtu atamsulubu?.
P
 
Hili lilikuwa ni ombi la zamani kumuomba Lissu asimsulubu Mwanamke, leo Lissu anarejea na atahutubia viwanja vya Mwembe Yanga Temeke, ombi hili sasa ni kwa kiongozi Mwanamke aliyepo sasa!.

Dear School mate Tundu Lissu, najua umepitia makubwa. Welcome back home. Nakuomba sana upunguze kidogo kuliishi jina lako, usimsumbue huyu Mama kama ulivyomsumbuaga yule Madam, Mwenyekiti wako Mbowe tayari ameisha onyesha uungwana na ustaarabu mkubwa, wa hali ya juu@, please do the same!, tufanye siasa za kiungwana na kistaarabu. Kubebwa bebeka, ukipedwa pendeka, ukishikwa shikamana, ukiaminiwa jiaminishe!.
Yaliyopita si ndwele, samehe, tugange yajayo tusonge mbele!.
Welcome back home.
Your school mate
Pasco
 
Umeamkaje mzee wangu
 
Wanabodi,
Leo nimelikumbuka bandiko hili kuhusu TL kukosesha mtu usingizi baada ya kuiangalia clip hii
View: https://youtu.be/UXFoyKtbEEA?si=l6IxoAUVEFFWXWSP
Usikute TL anamkosesha mtu usingizi!, halafu itokee TL ndie asimame nae 2025!, na alivyo hana break... si kuna mtu ataogeshwa .... kila uchao?.
Hapa ni ninauliza tuu!.

Ndio maana nimeshauri, kama mgombea wa urais wa chama kubwa 2025 ni mwanamke, then vyama vyote viweke wagombea urais wanawake wapambane na sio jitu dume zima lipambane ma majike!.

Hivyo nikapendekeza Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!

Na endapo wapinzani watakuwa hawana kabisa mwanamke ambaye ni match na mgombea wa chama kubwa hivyo ni lazima kumsimamisha mwanaume, then mgombea wa upinzani asiwe TL ili kumstahi mgombea mwanamke, maana jinsi TL asivyo na breki, hachelewi kumuogesha na mvua ya ... TL saizi yake alikuwa JPM na sio huyu Maza Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

hivyo nimeshauri mgombea wa upinzani awe Kama CCM Itamsimamisha Rais Samia 2025, Mnaonaje Freeman Mbowe Awe Mgombea wa Upinzani? Atapiga Ndege 3 kwa Jiwe Moja, Atavuna Wabunge Wengi ila... sababu ya kupendekeza FM ni kufuatia kukubali maridhiano na CCM kugawana nusu mkate, TL anayabeza maridhiano Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Hili mnalionaje?.

P
 
Tundu Lissu akichaguliwa kuwa Mwenyekiti Chadema, halafu 2025 akagombea urais... naomba nisimalizie.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…