Ni vizuri kabla ya kuwa rate hawa tuletee vigezo tutakavyo tumia kuwa chagua,kwa hali iliyopo sasa wote hawafai.Kama watanzania tunataka kutengeneza utamaduni mpya wa kufikiri na kutenda tunahitaji tujue matatizo yetu,vyanzo vya matatizo na namna ya kuyaondoa.Viongozi wa kisiasa tulionao ni matokeo ya watanzania wenyewe kuwa kabidhi vichwa wanasiasa wafikiri kwa niaba yetu,na hii ndo sababu ya wanasiasa kuwa na nguvu kushinda raia wenye nguvu.Na hii inafanya watanzania kutawaliwa na wanasiasa badala ya wao kuwatawala wanasiasa.Haya ni mawazo yangu,na ninaamini wote hawana jipya kwani wote wamejengwa na falsafa ya kitanzania inayosema "watu wanasema wasiyo yamaanisha na wanamaanisha wasiyo yasema"tafakari