Mheshimiwa kabla hujaondoka ulituachia laana au uliwaachia neema?

Mheshimiwa kabla hujaondoka ulituachia laana au uliwaachia neema?

Burungutu sandawesu

Senior Member
Joined
Sep 11, 2022
Posts
153
Reaction score
261
Kuna watu wananeemeka na kuwa matajiri zaidi baada ya kuondoka kwako na wale masikini wanakuwa masikini zaidi, je umetuachia laana au umewaachia neema, miaka yako michache sikuwahi pata shida ya maji na umeme hata kama vilikuepo sikatai lakini watendaji wanatumia siasa kwenye suala la maisha ya wananchi.

Upigaji umezidi na sasa ni waziwazi, tulikupenda na tilikuheshimu japo kuna muda ulituvuruga lakini watu tulifanya kazi na kuacha uvivu.

Lakini sasa kuna mtu mmoja ambaye yeye ni Mtanzania kuliko watanzania wote ametuambia kuwa tuhamie burundi kama hatutaki tozo, umekosa namna ya kuliweka sawa swala la tozo lieleweke mpaka utupeleke burundi.

Kwanza hatutoshi kule, lakini sifa zimezidi saaana kwa muheshimiwa wa sasa sisi wenyewe tunajiuliza anastahili?

Je, si ni neema tu hiyo imewaangukia, miradi mingi imesimama na report za CAG zimekua kawa kama series za kikorea unazisikia leo kesho wamezipotezea na hatujui suala limeishaje ndio ishapigwa hiyo.

Mheshimiwa muendee hata kwa ndoto tu umkumbushe, maana wanasiasa hawamsaidii sijui wanamdanganya au nini, ila shida tunapata sisi huku mtaani maharage kilo elfu nne sasa, maji ni kama ngumi ya ndoige tuu yakitoka kama yametoka yasipo toka kama yametoka tu bili ni ileile na maji yanayoka mara mbili kwa mwezi.

Tusamehe sisi Watanzania mh ila tuombee tupate maarifa akili zifunguke 2025 tusirudie matatizo,
 
Ila chuma alijua sana kuwanyoosha wapuuzi, Mpaka leo japokuwa amekufa lkn hao wapuuzi bado inawachoma.
 
Back
Top Bottom