Tangu uonekane pale Zakheim ukiwafurusha TBC, na kumwaga nondo jinsi CCM inavyowatesa watanzania kwa zaidi ya miaka mitano umekuwa kimya.
Umemuacha Lissu apambane peke yake, na sasa mgombea wetu ni kama amepanick,kwa hiyo anahitaji msaada wa mwenyekiti wa chama.
Maana wewe kuwepo kunaweza kumtuliza ili asiropoke maneno hovyo. Maana wengine wameanza kusema anakiuka maadili na sheria za uchaguzi,kwa kuanza kuropoka hovyo.
Mbona Zitto anagombea ubunge lakini anafanya kampeni huko kusini na Zanzibar. Pia na wewe ungana na Lissu ili kuongenza nguvu.