Mheshimiwa Nyangasa karibu Kigamboni anza na kupatikana Huduma ya Maji ya DAWASA na Tozo Daraja la Kigamboni

Mheshimiwa Nyangasa karibu Kigamboni anza na kupatikana Huduma ya Maji ya DAWASA na Tozo Daraja la Kigamboni

Joined
Jun 21, 2021
Posts
32
Reaction score
29
MHESHIMIWA NYANGASA KARIBU KIGAMBONI ANZA NA UFUMBUZI WA KUPATIKANA HUDUMA YA MAJI NA PILI TENGENEZA MIKAKATI YA SERIKALI KUONDOA TOZO ZA DARAJA LA KIGAMBONI KWA WANANCHI

Nianze kwa kuipongeza mamlaka ya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya, yaani Mheshimiwa Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kukuchagua wewe kuongoza Wilaya ya Kigamboni, tunamshukuru kwa kutupatia Tumaini jipya la maendeleo

Natambua umeisha anza kuchapa kazi na naomba ufanyie kazi kero kunwa mbili za wananchi wa Kigamboni ambazo ni kutokuwa na huduma ya maji ya Dawasa na kulipia shilingi 2000 kupita na gari kwenye Daraja la Kigamboni.

Kuhusu swala la maji, wananchi tunatambua serikali iliwekeza kuchimba visima vya maji maeneo ya Kimbiji toka mwaka 2016/17 na taarifa zinaonyesha maji yalipatikana. Je ni kwanini maji hayo hayaunganishwi kwenye mtandao wa DAWASA ili wakazi wa Kigamboni wapate huduma hiyo, mpaka sana hilo swala halina majibu zaidi ya kuwa story za miaka nenda rudi.

Utajiuliza kwanini jambo hili linaletwa kwako, ni kwa sababu ni swala la kimkakati na la ilani ya chama cha mapinduzi isipokuwa kigamboni kama Wilaya change mbunge wake alipopewa uwaziri anakuwa na majukumu ya ziada na kushindwa kusimamia baadhi ya maswala ya jimboni kwake.

Ukiwa kama msimamizi mkuu wa kamati ya siasa ya wilaya ninakuomba hili liwe kipaumbele chako. Kwa mkoa wa Dar es Salaam, biashara ya kuchmba visima imebakia Kigamboni tu na nafikiri hii sio sawa kuwatwisha wana kigamboni mzigo wa gharama za kuchimba maji yasiyo na uhakika wa ubora.

Jambo la pili ni kuhusiana na tozo za kuvusha magari katika Daraja la Kigamboni. Pamoja na kutambua kwamba daraja la Kigamboni limejengwa kwa ubia kati ya Serikali na mfuko wa mafao wa NSSF kwa makubaliano ya urudishwaji wa pesa za mradi itokane na mapato.

Nadhani huu ni mzigo mkubwa kwa wakazi wa Kigamboni na haundani na falsafa ya Serikali ya kujali maisha ya wananchi wake. Imefika wakati sasa wa kuishauri serikali iwalipe NSSF ili kuondoa mzigo huu wa wananchi. Hoja ijengwe kwa kuzingatia gharama za madaraja ya juu ya Ubungo, Tazara, Chang’ombe mataa, uhasibu, Busisi, Tanzanite n.k ambayo gharama za kuyajenga huenda zinashabihiana au hata kuzidi gharama za kujenga daraja la Kigamboni.

Hali ya uchumi wa miaka hiyo uliosababisha watu wa Kigamboni wakapewa mzigo wa kulipia gharama hizo si sawa na sasa ambapo uchumi wetu umekuwa na isitoshe gharama ya ujenzi imeishapungua kwa muda ambao daraja hilo limefanya kazi. Ni wito wangu tathmini ifanyike upya wa deni halisi na serikali ilichukue ikiwezekana hata kwa kuweka kwenye mafuta n.k tusije tengeneza utofauti kati ya sehemu moja na nyingine kwa huduma ambazo zinatolewa na serikali.

Vinginevyo gharama ya mafuta ishuke kwa wilaya ya Kigamboni ili kuwapa nafuu wakazi wa Kigamboni hususani wenye magari ili kuthamini mchango wao kwenye malipo ya daraja. Kwa sasa kila mmiliki analazimika kulipia shs 4000 kwa siku kwenda kazini na kurudi kwake ambayo ni sawa na shs 120,000 kwa mwezi na shs 1,440,000 kwa mwaka au milioni 14 kwa miaka 10, tumpunguzie gharama za maisha mtu huyu.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ni kweli mashauri haya ni majukumu ya mbunge ila kwa kuyatekeleza utajipambanua tofauti na wakuu wengi ambao kwao ubunifu ni kuweka watu ndani, kupanda magari ya kifahari, kuitwa waheshimiwa, kupigiwa saluti n.k huku mambo mengi ya maendeleo wakiwategemena watendaji wao wa chini ambao wanaishi kwa matumaini kwa wamekata tamaa ya kutopanda madaraja na kulipwa mishahara ile kwa muda usiojulikana. Chonde chonde mwanzo mgumu ila ukipatia mwanzo, hutoshindwa mbele. Kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yako.
 
Acha watu wachangie uchumi wa nchi! Upite darajani bure halafu pesa za kulipia gharama za huo ujenzi zitoke wapi? Au waongeze VAT? Au waongeze PAYE? Mtu kama hawezi kupita darajani akapite kwa pantoni kama nayo hawezi ahame toka kigamboni!
 
Kama maji ya kisima yaliyotapakaa Kigamboni yote tena bure yamekushinda utaweza bill za Dawasa,,... Unataka bure bure sasa Ile gharama ya Ujenzi na inatakiwa uelewe daraja halikujengwa Kwa hisani Bali kwasababu ya miradi mingi ya Nssf Kigamboni sasa hii miradi mliamua kuisimamisha sasa mnataka bure tena,hiyo fedha watarudisha vipi?!!..Huna huruma hata na wastafu duh
 
Back
Top Bottom