Mheshimiwa Rais Samia amejipambanua kimataifa kwa kuipa lugha ya Kiingereza umuhimu wake

Mheshimiwa Rais Samia amejipambanua kimataifa kwa kuipa lugha ya Kiingereza umuhimu wake

Huyu mama tumuongezee muda atawale maisha, naunga mkono hoja atake asitake ataongezwa
Ngoja mwimbo wa Taifa uanze kupotea Ikulu na baadala yake Taarab ndio italamaki

Hapo ndio utakuja mbio humu huku ukihema kuwa muhula wa mama uwe ni mmoja
 
Tunaipenda lugha yetu adhimu ya Kiswahili lakini hatuwezi kuipuuza lugha ya Kiingereza iliyotumika tangu ukoloni hadi 2015 ilipoanza kupoteza umaarufu.

Lugha zote ni muhimu and 'they perfom the same function'

View attachment 1736446
View attachment 1736447
Hii lugha wiki mbili zilizopita lilikuwa kosa la jinai kuisifu hadharani Kama ilivyokuwa kuchinja Mbuzi na kualika majirani kabla ya marehemu kuzikwa.
 
JF Home of great thinkers,sijutii kujiunga na JF.
 
MzeeBaba kuna tweet moja niliiona miaka yake ya mwanzomwanzo kwenye hatamu,
Aliingia chaka la 'Kinge' hadi aibu.
Na ndipo akaanza kuwa Mswahili halisi.
 
Kingereza ni kizuri lakini kwa watanzania, umuhimu wake hauna utofauti na wajumbe wakati wa kura za maoni CCM!
Yaani kujigamba kujua kingereza, kulisababisha Lissu aambulie kura kiduchu kutoka kwa wananchi! Tanzania ukijitia kujua na kuongea hiyo lugha unapondwa! Sijui kwa nini!
Mahera yupo sijamuona hata msibani.
 
Jiwe english ilikataa aisee
... Kwa kweli kilidunda! Naye akakichukia mazima to an extent ya kukifuta kabisa. Sijawahi kuona kitu cha aina hii kwa kweli. Solution ilikuwa ndogo tu learn, learn, learn. That simple!
 
Kwenye hili naomba ni comment Raisi aondoe ubaguzi shule zote za msingi za serikali ziwe English medium si baadhi ziwe english medium na zingine swahili medium wakati zote zinamilikiwa na serikali.Walimu huandaliwa kwa kiingereza ku switch sio big issue ni serikali tu kutangaza kuwa kuanzia leo shule zote ni English medium Walimu waliopo watageuka tu kufundisha kingereza .Shule zote za private walimu wanatoka vyuo vya ualimu vya serikali mbona wana perform? kiswahili kibaki tu kama somo msingi na O level na lugha ya taifa na mtu akitaka kulichukua kama speciality asome A level na chuo kikuu akafundishe nchi za SADDC na umoja wa Afrika walioamua kiswahili kuwa lugha ya Afrika

Tuko utandawazi
 
Raisi maadamu katanka ataondoa ubaguzi wa watoto wa viongozi wa serikali na chama na bunge na mahakana watoto wao kuwasomesha English Medium halafu watoto wa walalahoi waio wengi wanawakomalia wasome shule za kiswahili wakati wao wanajua umuhimu wa kiingereza

Ashughulikie hilo kumaliza tofauti ya watoto wa maskini kusoma shule za kiswahili wakati watoto wa viongozi wa CCM wa serikali na bunge na mahakama na viongozi wa upinzani watoto wao wanasoma kiingereza kuanzia chekechea ni English medium tu

Huo ubaguzi aumalize kwenye kipindi chake watoto wa wanyonge na maskini na wao wanahitaji English medium bila shaka naye atakuwa raisi wa wanyonge atashughulikia hilo kuondoa tofauti
 
Huyu mama Ni makini haijawahi tokea
Kifupi Ni chaguo la MUNGU
 
Hii lugha ilifanya watu washindwe kwenda ulaya
Watoto wa viongozi wa CCM na viongozi wa serikali na bunge na mahakama na viongozi wa upinzani watoto wao husoma English.Medium kuanzia Chekechea!!! za private

Kazi kwake kama Raisi kuhakikisha hiyo tofauti inaindoka kama alivyotamka ili kila mtoto awe na access ya kusoma English Medium kama hao watoto vigogo ili nao waende ulaya
 
Yaani asipobadilisha swahili Medium Schools kuwa English medium schools hili tamko lake halitakuwa na faida yoyote kwa Wanyonge na maskini wanaosomesha watoto wao swahili medium schools za selikali wasio na uwezo kusomesha watoto wao English Medium Schools
 
Back
Top Bottom