GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
ANGALIZO
Naomba kama unajijua kabisa kuwa uwezo wako wa kuona vitu vya umbali / unyeti / umuhimu wake basi katika huu ' Uzi ' kaa nao mbali kabisa na waachie wenye ' akili ' zao na ' Wachambuzi ' wa masuala haya ya Kijasusi ambao wapo ( tunao ) wengi humu na Sisi Mangumbaru na Mapopoma wengine tuwe watazamaji tu kuliko Kuchangia halafu ukajikuta umevapa / umekosea.
HOJA KUU
Nashukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba karibia awamu zote za nchi hii nilikuwepo japo ya Hayati Baba wa Taifa ilinikutia nikiwa bado katika Ndoo ya Kuogea na nalilia Uji wa Buruga ( namaanisha nikiwa bado Kichanga kabisa ) ila kwa awamu ya Mzee Mwinyi niliishuhudia bila kusahau ya Mzee Mkapa na ya Mzee Kikwete na sasa nipo hii ya Mheshimiwa Dkt. Magufuli natiririka na naserereka nayo.
Katika Awamu zote hizo sikuwahi hata Siku moja kuwasikia hao Watangulizi wake Rais Dkt. Magufuli wakiwa na tabia ya kupenda ' Kumtajataja ' au hata kupenda kuonyesha kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Idara Nyeti nchini ya Usalama wa Taifa ( TISS ) yupo eneo ambalo Wao wapo ila ilikuwa ni mpaka tu labda Mtu akutonye / akuambie.
Nimejuiuliza maswali mengi sana kwani Marais wote Wastaafu walikuwa hawapendi kuwatajataja Wakuregenzi wao Usalama wa Taifa ( TISS DG ) lakini kwa Awamu hii ya Gwala / Tano Rais Dkt. Magufuli anapenda mno ' Kumtaja ' na hata kupenda ' Kumuinua ' Kitini Mkurugenzi wa sasa Dkt. Modestus Kipilimba na bado sijapata jawabu / jibu ila najua kupitia ' Majiniasi ' waliotukuka wa Jamvi hili la JamiiForums leo nitayapata.
Sikuishia tu hapo kama kawaida yangu huwa napenda kwenda ' deep ' zaidi kufanya ' references ' na Mataifa mengine mbalimbali kuanzia na haya Jirani ( tunaofanana kwa Vingi ) kisha hupenda pia kuangalia na yale Mataifa makubwa ambayo yana uwezo mkubwa wa Kuanzia Uchumi, Kijeshi na Kiusalama kuliko Tanzania yetu hii na sijaona mahala ambapo Marais wao huwa wanawataja hovyo tena hadharani Wakurugenzi Wakuu wa Idara zao ' Nyeti ' za Usalama wa Taifa ila kwa Tanzania naona hii tabia inaanza Kuzoeleka.
Kwa maoni au mtazamo wangu mdogo tu ( mnaojua zaidi mtanisaidia ) kwa asili ya hizi nchi zetu tena ambazo zina ' Majaribu ' na ' Matatizo ' mengi ya Kimsingi huku kukiwa na ' Maadui ' wengi wa ndani na nje sidhani na siafiki kabisa tena kwa 100% kwa Wakurugenzi wetu hawa wa hii Idara / Taasisi muhimu kama si nyeti ya Usalama wa Taifa ( TISS ) kutajwatajwa hovyo kwa Watu na hata kujulikana kwakuwa Tanzania ya sasa imejaa Watu wa ajabu ajabu wenye ' maslahi ' yao ' hasi ' na nchi hii hivyo kuna uwezekano na Wao wakaanza Kumjua na Kumzoea kisha hali ikaja kuwa mbaya zaidi huko mbeleni.
Na sidhani pia kama hata ' Kiuweledi ' hivi anavyofanya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. Magufuli la kupenda ' Kumtajataja ' Mkurugenzi Mkuu wa Idara / Taasisi ya Usalama wa Taifa ( TISS DG ) Dkt. Kipilimba ni sahihi na kama itapendeza nadhani Watu wa ' Itifaki ' ambao nina uhakika kuwa wengi wenu tunatiririka na kuserereka pamoja 24/7 hapa JamiiForums hili mtaliangalia kwa hayo mapana yake ili utaratibu ule ule uliozoeleka wa zamani wa hawa Wakurugenzi kutojulikana sana au kutajwatajwa hovyo uendelee kwani Kwangu Mimi kwa ' Mazingira ' ya nchi yetu ulikuwa ni utaratibu murua / mujarab / sahihi kabisa kuliko huu wa sasa aliouanzisha Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. Magufuli.
Huu ulikuwa ni mtizamo wangu Mimi kama GENTAMYCINE ila nitashukuru na Watu wengine nao wakija hapa wakichangia huku wale ambao ' watanikosoa ' basi wanikosoe ha ' Hoja ' nzito nzito kwani hata Mimi nataka Kujifunza jambo hapa kutokana na kwamba yawezekana huu utaratibu wa sasa ukawa ndiyo sahihi kuliko ule ambalo nimeukariri / nimeuzoea. Nia na madhamuni tupate afya ya Kimjadala na ya Kimantiki juu ya hili ' Suala ' kusudi mwisho wa Siku wote tupate ' maarifa ' na ' ufahamu ' zaidi.
Karibuni!
Nawasilisha.