Mheshimiwa Rais sidhani kama kupenda Kwako kila mara ' Kumtajataja ' hadharani TISS DG Dkt. Kipilimba ni sawa Kiuweledi

Uandishi mbovu
 
Ukiwa hujiamini lazima utafikiria nguvu toka nje ya akili na mwili wako kukabiliana na watu wengine unaowahofia ktk maisha ya kila siku.
 
Magu anapenda ubabe wa kuogopwa sana huku akijua kariba ya kumtisha mtu hivihivi kwammaneno kama ilivyokuwa kwa Julius hana. Pia kujenga hoja za kushawishi hawezi, ndo maana ili aogopwe anatumia sana vyombo vya ulinzi na usalama mbele ya raia au watu anaohisi wanapuuza ujumbe wake. Katika awamu hii majina kama...mabeo, kabirimba.. yanasikika sana kutoka mdomoni mwake badala ya raia wa kawaida kukutana nayo
kwenye habari za kiuchunguzi za magazeti au kutoyasikia kabisa ukiachana na anapoteuliwa au kustaafu.
 
Kwa ulimwengu wa sasa hata asiotajwa tajwa Kama mtu anataka kujua habari zake atazijua tu. Kumbuka huyu sio undercoverd maana uteuzi wake ni public announced.
 
Mkuu GENTAMYCINE unaishi dunia ya juzi saba where names and faces of intelligence chiefs used to be concealed. Hiyo ilikuwa hapo zamani za kale sio enzi hizi. In short ni zilipendwa! Humjui chief wa CIA, MI6 na wengine kama walivyotajwa na wanawataja JF? Wewe kweli ni zilipendwa!!

 

Jk alikuwa anamtaja Sana bwana Othman na kwa kiongozi mkubwa sio siri coz huwa anateuliwa na kuapishwa live kila mtu akiangalia

Na kwenye dhifa Zote za serikali utamjua tu kiongozi mkuu wa tiss coz wanakaa mstari mmoja viongozi wote wa ulinzi
 
Acha uongo!
 

Mkuu, bwana mkubwa anawasiwasi. Anajaribu kuwaogopesha wanaomkosoa. Time will come when every tree will be a death trap. Thats the end.

Hii inakuonyesha jiwe hana Amani, anajua ana madhambi yeke makubwa na watt wanajua. na wamemkalia kimya. Kuna siku yake
 
Kati ya idara ambayo mambo yake yanafichwa sana(na raia kuona ni sawa tu) ni hii ,kuanzia ajira zake,bajeti,watendaji wake wakuu na jinsi inavyofanya kazi zake hakuna uwazi wala haieleweki.Sijui sababu za kufanya hivi ni nini wakati hii ni taasisi ya umma,mataifa makubwa ya magharibi yaliyoendelea na yenye kukabaliana na vitisho vikubwa vya kiusalama kila siku idara zao za kijasusi zimeweka wazi angalau taarifa zao awali/msingi(ajira zao wanatangaza, watendaji wao wanajulikana na huthibitishwa na bunge ,ofisi zao zinajulikana zilipo na bajeti zao za jumla zinaidhinishwa na bunge) mataifa mengi fukara na ya kidikteta wameamua kuziweka idara hizi gizani na hii imeondoa weledi wao kabisa na kubaki ni vyombo vya kuhakikisha tawala zinabaki madarakani kwa njia za vitisho na mateso kwa wenye mawazo mbadala.
Hii ni kusema kwamba swali lako wala halifai kwa mjadala wenye afya wenye lengo la kuboresha hali ya mambo ila linatupeleka tu gizani zaidi.
 
Mkuu mleta mada GENTAMYCINE upo sahihi asilimia 100% ndy maana hata ujumbe/ushauri wako wa upendeleo wa mkuu wetu (kupendelea UDSM kama hamna vyuo vingine) umefika na kupokelewa kwa mikono yote (Nafikiri utakuwa umemsikia mkuu wa kaya)

Hii tunasema ni defense mechanism anavyosema kuwa wakuu wa vyombo vya usalama na mkuu wa Usalama wa Taifa ( TISS ),sasa kwa hali tuliyonayo hapa Tanzania kwa sasa haitakiwi kutajwa kabisa yeye aendeleee na kuwataja wengine lakini aachane kabisa na vyombo vya ulinzi na Usalama wa Taifa ( TISS ).

Hawa wote ni watu ambao hawatakiwi kuzoeleka machoni pa jamii japo wanajulikana lakini siyo kutajwa kwenye public.

Nafikiri ujumbe huu utamfikia kupitia mtiririko huu wa hapa jamvi la jamiiForum
 
Natabiri atampa teuzi au nafasi kubwa sana kwa njia tu kumtoa kwenye hiyo nafasi. Kwa hiyo hapo anaonesha kuwa wako karibu na wanashibana. Labda ndiye PM ajaye
 


Mnalipwa kwa umbea huu? Tuanzie hapo.
 


Hizi ni hisia za umbea na uchochezi! Kuna kitu unataka watu wakusuport ...... maana waliokupinga unawaita mapopoma!
 
Katika mataifa yote makini huwezi kusikia mission yoyote ikihusishwa na usalama wa taifa. Usalama wa taifa hufanya mission nyinging sana lakini mwisho wake utasikia "Jeshi la Polisi limekamata, au TANESCO Imegundua, au wasamaria wema wawataja waharifu/majambazi, au wanafunzi wa chuo fulani waibua madudu, au ofisi ya mkaguzi mkuu wa serikali yaibua madudu, au Speaker wabunge atoa utaratibu mpya, au Benki kuu yagundua au T.R.A yagundua mianya inayotumiwa na wafanyabiashara kukwepa kodi au Rais amtumbua kiongozi fulani au amteua fulani.
Ukiangalia, asilimia karibu 80 ya hayo yote hufanywa na idara ya Usalama wa taifa lakini hutumia mamlaka tofauti kuelezea kazi zao, wao si kazi yao kujieleza, wao hufanya lakini mwisho huiunganisha mamlaka husika bila mamlaka hiyo kujua kuwa inafanya kazi ya idara ya usalama. Idara huendelea kufanya kazi zake kwa ukimwa na usiri kama vile haipo. Mkuu wa Idara si mtu wa kuonekana onekana hata kwenye misafara ya rais.
Kitendo anachokifanya rais Magufuli kinaifanya idara ya usalama isomeke sana, wataalamu inawawia rahisi sana kuunganisha dots.
 
Mkuu wa CIA ya USA anaenda hadi kushtakiwa sisi hapa eti hata kumataja ni kosa! Alaa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…