Mheshimiwa Rais sidhani kama kupenda Kwako kila mara ' Kumtajataja ' hadharani TISS DG Dkt. Kipilimba ni sawa Kiuweledi

Mkwara mwingi basi hatujibu ila yupo sawa.
 
Hii ina maana mkuu Wa nchi Hawa watu wengine kwake ni kigumu kuwajua hii ina maana hata mwanawane anaweza kuwa jasusi na asimjue?
Nalog off
 
Sio Madafa ? Bila shaka yupo Italy
 
Huyo Dgis ni Public Figure hata sheria ya mwaka 1996 inaeleza na kutaja majukumu yake. Sasa Rais wa awamu ya tano kama umefuatilia vizuri amekuwa akiambatana nao katika function nyingi za serikali na pia amekuwa akiwataja au kuwatambulisha pamoja na Igp au Cdf. Huo ni utaratibu ambao umempendeza Rais JPM.

Katika kipindi cha awamu ya nne Rais Mstaafu JK Kikwete yeye alikuwa anapenda kusalimia wananchi katika function zake nyingi kwa kugonga nao mikono. Hili ni hatari kiusalama sababu adui anaweza kutumia mwanya huo kumdhuru Kiongozi wetu Mkuu. Cha msingi katika relationship kati ya Rais na Wakuu wa Dola inabidi tahadhari ichukuliwe na Viongozi hawa wa dola. Wanatakiwa wawe makini zaidi kuliko amiri jeshi mkuu maana wao ndio wana mamlaka ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa Rais.

Kutaja au kujulikana kwake siyo ishu. Ishu ni kuhakikisha tunakuwa salama kiusalama na kiulinzi.

Kumbuka Katiba Pendekezwa ya Warioba ilipendekeza hadi upatikanaji wa Dgis, Cdf na Igp kuwa baada ya Rais kupendekeza majina matatu, wanakwenda katika Bunge la JMT kujieleza na kuahidi watafanya nini yaani kwa kifupi wanawashawishi wabunge ili kura zikipigwa basi jina moja linapitishwa na kuwa kiongozi wa chombo hicho. Sasa ukiangalia kwa undani endapo huu utaratibu ungepita ingekuwa zaidi ya Hoja yako kwamba JPM anawataja hadharani.
 
Vipi ikiwa anafanya hivyo kuwapoteza watu maboya? Labda DG halisi sio huyo unaemjua wewe (aliyetajwa humu)?
 
no offence mtoa mada, mbona hata kwa kikwete hafla zake nyingi rasheed othman hakuacha kuhudhuria.. binafsi sioni shida make yule sio mtu wa kujificha hata mimi leo nikitaka kumjua sio lazima nimjue kupitia kutajwa na magufuli. na mtoa mada ulijua kabisa kama sio kutajataja maneno mengi yasokua na maana; popoma, great thinker, ujasusi, tukuka, gentamycine, tiss, ngumbaru, dg etc wasomaji wangekushtukia kama jamaa hua ni wale nzi wakubwa wa chooni tuu..
 
Anawajua wote! Kwa level aliopo kwa sasa hana sehemu ambayo hana access nayo,ni kama vile tu alivoomba alete orodha ya watumishi wote wa benki kuu ya tanzania na akapewa majina yote ya watu hao,sasa atashindwa kuomba orodha ya hawa na kuwajua kwa majina,sura na mpaka kabila mmoja baada ya mwingine.
 
Useless caution. Una akili ya kizamani ya kuamini usalama ni siri na njama. Eti usalama ni kuzuia kupiga picha, nk. Huyo mtu hatakiwi iwe ni siri! Boss wa CIA anafahamika hadi hapo ulipo na hata mtandaoni jina lake linaonekana. Hizi siyo enzi za usalama wa siri na kutojulikana. Usipojulikana unafanyakazi na nani? Ukikosea nani akukosoe bila kukufahamu?
 
Huyu anampenda sana maana ndiye aliyemsaidia wizi ka kura mpaka akaukwaa urais, hivyo anajipendekeza sana ili isije siku moja siri ikavuja. Nchi nyingine zina tume huru za uchaguzi
 
Mimi nina haya machache kutokana na uwezo wangu mdogo katika mambo haya,

Kwanza niseme awamu zote nimekuwepo awamu ya kwanza nilikuwa shule na zilizofuata na hii hapa ya Tano kwanza haikuwa Rahisi kujua Mkurugenzi wa TISS au kuwajua watumishi wao hata pale walipotaka kusafirisha mkurugenzi wao usingeweza kujua ila sasa mavimurimuri wanawazidi hata Traffic hili nikosa maana kwa sasa na wao wanataka watambulike kuwa wao ndo TISS hivyo naona utofauti mkubwa sana,na wakati wakumpata mkurugenzi wao kulikuwa na vetting ya Directories RSO,DSO,etc ya TISS na ya kamati kuu za ulinzi na usalama anapelekewa Rais anateua katika majina aliyopewa,tofauti na sasa anachagua kutokana na matakwa yake hata wakuu wa majeshi as well.Naomba mchukulie haya maelezo kama binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…