omugabire
Senior Member
- Jun 17, 2019
- 128
- 174
Mheshimiwa Rais utakapoanza kudhuru kwa wakuu wa wilaya usimsahau mkuu wa wilaya ya ukerewe Bw. Lucas magembe
Mkuu huyu wa wilaya tangu apangiwe majukumu yake katika wilaya ya ukerewe amekuwa ni mtu mwenye migogoro isiyo isha baina yake na wananchi na viongozi wa dini.
Tangu kuripoti kwake mwishoni mwa 2018;
1. Ameingia kwenye mgogoro wa ardhi na kanisa katoliki hadi mapadri wakaandika waraka wa kutoshirikiana naye kwa jambo lolote.
2. Ameingia kwenye mgogoro wa ardhi na wanchi wa kata ya Nkilizya
3. Ameingia kwenye mgogoro na wavuvi kwenye operesheni sangara.
4. Ameingia kwenye mgogoro na wananchi wa ukara kipindi cha uchaguzi hadi kupelekea umwagaji damu.
5. Ameingia kwenye mgogoro na kanisa la waadventista wasabato.
6. Ameingia kwenye mgogoro na wananchi wa kata ya kagunguli na maeneo mengine kwenye ukusanyi wa pesa za michango ya ujenzi wa madarasa hivi karibuni.
Katika mgogoro huu, mkuu wa wilaya anatisha wananchi na kutumia jeshi la polisi kukusanya michango ya ujenzi wa madarasa kinyume na utaratibu. Na wananchi wanaodai risti au kuhoji mwenendo huo wa ukusanyaji michango amekuwa akiwaweka rumande na kuwabambikia kosa la kugomesha zoezi ambapo kutoka ina walazimu kutoa kiasi cha shillingi laki moja ambayo pia haitolewi risti.
Mheshimiwa Rais katika kujiridhisha na hizi tuhuma nakushauri uunde timu yako toka ikulu ije kuzichunguza na hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya huyu DC maana matendo kauli na maamuzi yake ya kibabe ni vithibitisho tosha kwamba hafai kuwepo kwenye hiyo nafasi.