Nilisha sema hapa jamvini kuwa katika vitu hatari na vibaya kwa mustakbali wa Elimu ya Tanzania ni TUME YA PINDA. Hebu tuliangalie hili suala kwa Mawanda yake, katika mfumo wetu huu wa Elimu unaotolewa na Walimu waliokata tamaa kwa kazi yao, ukosefu wa vitabu bora, ukosefu wa maabara , utitili wa shule za kata zenye wanafunzi ambao hata hawajui kusoma na kuandika, uhaba wa walimu, kushushwa kwa alama za ufaulu hadi alama 70 drs la 7, kuondolewa kwa mitihani ya kidato cha pili. Hayo na mengine mengi ,tulitegemea watoto wafaulu mtihani wa kidato cha nne kwa muujiza gani? Tume ya Pinda ni janga kubwa kwani imelenga kuficha madhaifu ya serikali na kulinda nafasi za viongozi. Baraza la Mtihani kilikuwa ni chombo pekee ambacho kilikuwa bado Kimesimama kwenye Misingi ya kujenga Elimu pamoja na mageuzi makubwa yaliyojitokeza kwenye sekta Ya Elimu nchini. Namshauri dr. Ndalichako ajiuzulu kulinda heshima yake kwani heshima ya chombo anachokiongo imeshapopolewa mawe na wanasiasa.