Mheshimiwa waziri mkuu Tunakushukuru ubarikiwe na tume yako

Mheshimiwa waziri mkuu Tunakushukuru ubarikiwe na tume yako

Nikhil

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
361
Reaction score
120
Wakuu nafkiru mko good.
Wana jf nimetupua thred hii kutokana na influence ya shukrani nyingi kitaa wake waliopoteza matumaini ya advance wanamshukuru sana waziri na tume yake kwa kufichua maasi ya kuongeza madaraja ya ufaulu.
Wewe kama mdau unapenda kumueleza nini pinda pamoja na tume yake?
 
Nadhani lengo nikuonesha tume haikuundwa bure! Prof Mchome must be knowing what he is suggesting!
 
Tukisema Tunajivunia Jeuri ya Chama ndio hii, Chama sikivu kinazaa serikali sikivu inayopata kuongoza Raia Sikivu.Kidumu chama cha Mapinduzi, kidumu chama Tawala Milele ameen!
 
Necta wameiingiza serikali hasara na wananchi kwa ujumla kutokana na uzembe wake wa kutozingatia kanuni na taratibu za kupanga madaraja. namshauri wahusika wa hasara hii waachie ngazi wenyewe au wawajibishwe.
 
Sioni kama kuna lolote ila nikutaka tu kuzalisha wasomi mbumbumbu mbeleni kwan navojua watasukumiwamo tu kama magunia!
Tunaelekea kubaya kielimu. Na ninawashangaa sana mnaofurahia kupangwa upya kwa grade za ufaulu
 
Huu ni mchezo tunachezewa na wasiasa bila sie kujua. Necta walishatoa tamko mapema walitumia grade za zamani sio mpya. Sasa wanasiasa kwa kukwepa lawama na kuoneana wanajali na kufunika kombe wamerudisha lawama kwa necta. Sasa je necta nao wakisisitiza tamko lao walilolitoa maana kuna wale walionda kurudia kusahisha na grade zilizotumia ni za zamani walifeli zaidi. Siasi ktk elimu yetu inakufa.
 
hapo lazima lungu lidondokee necta hata kama usahihishaji ulikuwa ni sehemu ya mgomo wa waalimu elimu imekuwa vululu mbulula
 
Nilisha sema hapa jamvini kuwa katika vitu hatari na vibaya kwa mustakbali wa Elimu ya Tanzania ni TUME YA PINDA. Hebu tuliangalie hili suala kwa Mawanda yake, katika mfumo wetu huu wa Elimu unaotolewa na Walimu waliokata tamaa kwa kazi yao, ukosefu wa vitabu bora, ukosefu wa maabara , utitili wa shule za kata zenye wanafunzi ambao hata hawajui kusoma na kuandika, uhaba wa walimu, kushushwa kwa alama za ufaulu hadi alama 70 drs la 7, kuondolewa kwa mitihani ya kidato cha pili. Hayo na mengine mengi ,tulitegemea watoto wafaulu mtihani wa kidato cha nne kwa muujiza gani? Tume ya Pinda ni janga kubwa kwani imelenga kuficha madhaifu ya serikali na kulinda nafasi za viongozi. Baraza la Mtihani kilikuwa ni chombo pekee ambacho kilikuwa bado Kimesimama kwenye Misingi ya kujenga Elimu pamoja na mageuzi makubwa yaliyojitokeza kwenye sekta Ya Elimu nchini. Namshauri dr. Ndalichako ajiuzulu kulinda heshima yake kwani heshima ya chombo anachokiongo imeshapopolewa mawe na wanasiasa.
 
Sasa naamini watz wengi ni simple-minded, they will swallow almost every cra.p thrown at them/
 
Wale waliojiua inamaana imeshakula kwao!!

Kama kweli kuna madudu yamefanya na NECTA basi kimbunga hichi mama Ndalichako haponi.
 
Mmh hili jambo zito ndugu zangu.
Je, nani atasahihisha nani?
Je, waliofaulu wakifeli itakuaje?
Je, kama kashfa ni kufeli inamaana watafanya kila jambo ili kiwango cha ufaulu kipande?
 
Wakuu nafkiru mko good.
Wana jf nimetupua thred hii kutokana na influence ya shukrani nyingi kitaa wake waliopoteza matumaini ya advance wanamshukuru sana waziri na tume yake kwa kufichua maasi ya kuongeza madaraja ya ufaulu.
Wewe kama mdau unapenda kumueleza nini pinda pamoja na tume yake?
Nenda kajifunze kusoma na kuandika ndio uje hapa jamvini....au na wewe ndio wale waliochora mazombi afu wanangojea mtihani urudiwe wapate div 1???
 
Wakuu nafkiru mko good.
Wana jf nimetupua thred hii kutokana na influence ya shukrani nyingi kitaa wake waliopoteza matumaini ya advance wanamshukuru sana waziri na tume yake kwa kufichua maasi ya kuongeza madaraja ya ufaulu.
Wewe kama mdau unapenda kumueleza nini pinda pamoja na tume yake?
Tume imeshafanya kazi yake sasa subiri watakaorudia kumark upya hizo paper maana kila mmoja na kazi yake. lakini mpaka tulipofika kwa kazi ya tume imefanya kazi yake kwa sehemu kubwa sana
 
Watanzania wengi tunapenda urahisi katika kilakitu, NECTA wanajitahidi sana kuhakikisha elimu yetu inakuwa bora, lakini wanasiasa wanaharibu. Watu wamesha sahau hutuba ya JK na Kawamba kuhusu hayo matokeo ya mitihani, leo wanasiasa wanakuja na kauli nyingine watu tumeshabadili mwelekeo.
 
Back
Top Bottom