Zitto kuwekwa kitako na wapinzani Maulid Ahmed
HabariLeo; Tuesday,January 01, 2008 @19:02
MALUMBANO kati ya Spika Samuel Sitta na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, juu ya barua ya adhabu ya mbunge huyo, yameingia sura mpya kwani sasa Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa Kambi ya Upinzani itakutana na Zitto kwa ajili ya kumshauri juu ya suala hilo.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni ambaye ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF), alisema kamati hiyo itakutana na Zitto ili kumshauri juu ya barua yake aliyomuandikia Spika akilalamika kutotendewa haki kwa kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge pamoja na Spika alivyomjibu.
Mimi nimeipata jana nakala ya barua ya Zitto na nimeshampigia kumuambia kuwa tutakutana naye katika Kamati ya Uongozi kushauriana naye, alisema Hamad. Alisema kamati hiyo itakutana wakati wowote kuanzia Januari 14, mwaka huu ambao wabunge watakuwapo mkoani Dar es Salaam kujiandaa kuhudhuria kikao cha Bunge kitakachoanza Januari 29, mwaka huu.
Akizungumzia maoni yake binafsi, Hamad alisema binafsi ningeshauri Spika kwa upande wake aliache jambo hili liishe na Zitto naye kwake liishe na kusiwe na malumbano yoyote. Desemba 24, mwaka jana, Zitto alimwandikia barua Spika, akitaka kuipitia upya adhabu ya kumsimamisha kutokana na kwamba imesababisha adhalilike na kushushiwa hadhi ndani na nje ya nchi.
Alidai adhabu hiyo aliyopewa haikuwa halali kutokana na kutofuata Kanuni za Bunge na kutopewa nafasi ya kujitetea. Sambamba na hilo, anataka Spika Sitta na mawaziri wengine kadhaa wachukuliwe hatua kwa madai walinukuliwa na vyombo vya habari wakisema yeye ni mwongo bila madai hayo kuthibitishwa.
Hata hivyo, katika majibu yake, Spika alilikataa ombi hilo na kuahidi kuifikisha barua ya mbunge huyo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Sitta ameahidi kufikisha barua hiyo ambayo sasa haitashughulikiwa na Bunge, kutokana na maneno yaliyotumiwa na Zitto kujaa ufedhuli na ubabe dhidi ya Bunge kama taasisi na dhidi ya viongozi wa Bunge na Spika.
Katika taarifa ya majibu ya Spika Sitta iliyotolewa na Katibu wake, Daniel Eliufoo, ilisema kuwa barua hiyo ya Zitto itapelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kupata ushauri wake. Hata hivyo, hakusema lini ataipeleka barua hiyo zaidi ya kudai utakapofika wakati muafaka.
Spika alisema mbunge huyo kwa tiketi ya Chadema, ana hiari ya kwenda mahakamani ikiwa anadhani hatua hiyo itamsaidia kupata haki yake aliyonyimwa na Bunge. Katika majibu yake, Spika aliyeeleza kusikitishwa na maneno yaliyotumika yaliyojaa kiburi na fedhuli dhidi ya Bunge na viongozi wake, alisema barua ya Zitto ya rufaa si ya mbunge, bali ni waraka wa propaganda binafsi za kisiasa.
Zitto alisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge Agosti 14, mwaka jana kwa madai ya kusema uwongo dhidi ya Waziri wa Nidhati na Madini, Nazir Karamagi, kuhusiana na mkataba wa madini wa mgodi wa Buzwagi. Adhabu hiyo imekwisha na anatarajiwa
mie mwenzenu bado sijaelewa hii issue,Mheshimiwa anasema ndio kwanza ameipata,mheshimiwa ZITTO anasema inawezekana mkuu 6 au HR ndio waloitoa ktk net,SO WHICH IS WHICH............hebu wajuzi wa MAMBO TUWEKENI SAWA HAPA.