Mheshimu anaye kudai

Mheshimu anaye kudai

Umeishiwa kodi ya nyumba unahamgaika, umezidisha miezi mitatu, madalali wanapishana kuwaleta wateja nyumbani kwako. Wateja wanaingizwa vyumbani hadi kwenye chumba unacholala.

Hatufahamiani, umenifuata PM, umenipeleka hadi home kwako, umenitambulisha kwa mkeo na watoto.

Kwa machozi umeniomba msaada mbele ya mkeo. Nikawaandia cheque ili mlipe rent ya mwaka mzima.

Sikukuambia tarehe ya kunilipa ila nilikwambia ukipata pesa nirudishie.

Sasa wewe umepata pesa, kila siku ni sikukuu. Safari za mbugani, safari za nje ya nchi na bata kama lote,sikukatazi, lakini kwanini unanitag kwenye picha zako za Facebook?

Kuwa na heshima kwa watu waliokusaidia kwenye dhiki zako
Kuna mtu alikua ananidai, hata muda wa kumlipa haujafika bado nashangaa siku hiyo akanitumia meseji "we endelea kunenepa tu wakati nakudai!" Nilikasirika sana siku ile ile nikaenda kukopa hela kwa mtu mwingine nikamlipa.
 
Back
Top Bottom