Me too
JF-Expert Member
- Feb 9, 2015
- 7,388
- 9,333
Wale waangalizi wa Mali za wazee ambapo huteuliwa abaki kijijini ili kulinda ardhi na Mali zake pindi wazee wanapofariki kisha wenzake wanaenda mjini kujichanganya na maisha ya kimataifa.
Kama mwangalizi huyo ameishi hapo mpaka amekuwa na wajukuu tangu mufiwe na wazee na hakuna hata kitu kilichoharibika zaidi amekuwa akipaboresha mwenyewe huku Dada / kaka zake wako wanainjoi keki ya kimataifa na wameshapasahau kijijini nawaambia mumheshimu sana yule mwangalizi wa mirathi yeye na uzao wake, asingekuwa yeye leo hii jina la wazee wenu lingeshafutika mda.
Unajua mwangalizi huyo anakumbana na mangapi kisa kulinda ardhi ya wazee na yeye kusahau kujiwekeza kwake?
Hivi unaelewa shida ya kuzaliwa, kukulia, kuzeeka na watoto wako ukiwa kijijini hujabadiri mandhari ya maisha?
Unajua kasumba anazokutana Nazo dhidi ya kuitetea ardhi?
Siku akiwagusa mjichange mumuinue Kule kijijini mnampoza na matshirt km ya le- mutuz, mwangalizi huyo anaona isiwe tabu wenzangu wamekolea na maisha ya mjini.
Nawaambieni tu mnapokwenda kijijini msilete ubabe kwenye uzao wa yule mwangalizi na hata mwangalizi wa ardhi pia,,, tumia busara . sio upo mjini umesikia kauza miti ya mbao yote na amepanda mingine wewe kazi yako ni kupiga mahesabu hela aliyoipata mgawane, je! Analeaje watoto? Je! Mshara wako huko mjini mbona yeye haujui?.
Sasa ole yule mwangalizi kama alikuwa mwanamke akafa akawaacha watoto na wajukuu bahati mbaya aliemzalishaga alishatangulia mbele za haki na ndugu hawawatambui watoto hao. Kwa ujuaji wenu mnatoka huko mijini mmeshaprint na matshrt ya msibani, mazishi yameisha mnaanza kuwasambaratisha uzao wa marehemu wakatafute ndugu zao upande wa baba hatutaki makabila mapya, kwakuwa Dada yetu amefariki nyie sio damu yetu ila damu yenu ipo upande wa baba zenu, hivo tunawapa mda muondoke hapa, mbaya zaidi badala nje mkae nyie mnaweka mlinzi awe anawapa taarifa za hapo kijijini pindi muwapo mijini.
Ukabila haufai, kisa Dada yako kaolewa na mmakuwa na nyie ni wahehe ( samahani ni mifano tu ya makabila ) watoto wake hamuwatambui Dada yenu mnamtambua. Tumieni busara na mumuheshimu sana yule mwangalizi wa ardhi ya wazee hakuna asiependa starehe za mjini