Standards Person
JF-Expert Member
- Apr 22, 2021
- 672
- 860
Wanajukwaa habari zenu.
Sitaandika sana, ninajitahidi kufupisha mada yangu.
Kwamuda sasa imekuepo tabia kwa baadhi ya viongozi wetu wa dini kuonekana kila kwenye matukio ya kitaifa kama vile Dodoma, Dar es Salaam nk.
Jambo hili naona sio jema sana hasa kwa viongozi hao wa kiroho. Wanaweza wakajikuta wanatumikia mhimili serikali bila wao kujua. Hili linaweza kujitokeza kwa hofu,kujipendekeza au kutaka dolari.
Watu hao waliogeuka waendesha maombi kwenye mikutano mbalimbali wananiacha njia panda kwani nchi sio lazima iombewe kwenye majukwaa ya kisiasa pekee tena na watu walewale na maeneo yakiwa tofauti.
Nimetafakari kwamba kwanini mhimili wa kuishauri na kuisimamia serikali hauongozwi kwa dua za mashehe,mapadri,wachunhaji na maaskofu.
Mhimili huo una dua yake tangu naanza kuliona bunge. Mbona bunge halijakufa? Tena kama kuna sehemu inahitajika viongozi wa dini ili Ndugai na Tulia waone aibu hakika ni bungeni.
Alitakiwa mufti, mapadri na maaskofu wakakodolee macho kiti cha spika na wabunge watukanaji ili waache mizengwe, kuzozana, kudemka na hatimae haki itendeke.
Sasa huko Mahakamani ndio ilitakiwa viongozi wakiroho wakaombe,wafunge na kufungulia huko maana malalamiko ni mengi.
Hata hao viongozi wakiroho wamelalamika mara kadhaa kwamba wanaonewa kuanzia polisi kuwabambikia kesi na mahakama kutotenda haki. Kwanini hakuna dua ya viongozi wa kiroho huko mahakamani na kwenye vituo vya polisi?
Je, nafasi ya waabudu mizimu ipo wapi kwenye mhimili serikali? Au watu wa kimila wametengwa mpaka yakitokea majanga ya asili kama kimbunga, kukosekana mvua, vifo nk
Maoni yangu
Mhimili huu uwaache viongozi wa dini waendelee na majukumu yao kwani kwakutembea nao kila mahali mnaligawa taifa kwani hao viongozi wa kiroho wanajikuta kuonesha dhahirimapenzi makubwa kwa mhimili fulani. Akitokea mfano siku muft au mkuu wa kanisa akawa kwenye mkutano wa kisiasa wa chama kingine anaonekana muasi. Tuliona na tunazidi kuona.
Hivyo mhimili serikali usijawe na hofu utimizetu majukumu yake bila kuandamana na viongozi wa kiroho. Serikali kueni na dua yenu kama vile bunge na iwe inasomwa na mtu maalum hata Gerso Msigwa(kutokana na nafasi yake) kwani yeye ndio anatembea na mh. Rais.