Wahindi hasa hawa wajukuu wa wale waliokuja kujenga reli ni wabaguzi sana.Katika suala la yule mhindi aliyepewa mkong'oto ni kama somo ili ajue kuheshimu watu.
Unafikiria kiurahisi!
Kwahio wahindi wawaogope weusi, wakiwaona weusi wanahofia kupigwa.
Matokeo= wahindi watahama, je wanaodhirika tena ni kina nani?
Waswahili walioletewa maduka jirani.
Itabidi sasa waswahili kwa hizo bidhaa wakazinunue Nairobi
Hapo ume solve problem?
Tuangalie pande mbili,
Mhindi kumhisi mweusi kuwa mwizi si vizuri na mweusi kumpiga mhindi kwasababu kahisiwa mwizi sio vizuri.
Mswahili angeshitaki kama anaona anaonewa, na mhindi kama anaona anamhisi mweusi ni mwizi angemshitaki. sheria ndio zinazoamua
Hebu angalia hii kuhusu mambo ya sisi waswahili kuona kwamba kumpiga mtu ndio suluhisho.
Mgoni ampigia kelele za wizi mwenye mke
2008-05-29 11:17:18
Na Romana Mallya
Mchinja nyama mkazi wa Vingunguti kwa Kombo, Bw. Sokoine Mtunda, ameuawa na wananchi wenye hasira baada ya mgoni wake kumpigia kelele za mwizi.
Mtunda anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 20 na 25, alikutwa na mauti hayo baada ya kumhisi mtu aliyefahamika kwa jina moja la Hussein kuwa anamwibia mke wake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Bw. Faustine Shilogile, alimtaja mwanamke anayedaiwa kusababisha kifo hicho kuwa ni Bi. Muta Mazengo (25).
Kamanda Shilogile, alisema inadaiwa kuwa, mtuhumiwa huyo kabla ya kufikia hatua hiyo, alimnunulia Bi. Muta, doti mbili za khanga.
Alisema tukio hilo lilitokea juzi usiku eneo la Vingunguti, jijini Dar es Salaam.
Kamanda Shilogile alisema Mtunda aliporudi nyumbani kwake, alimkuta mke wake akiwa na nguo hizo ambazo hazifahamu.
Alisema baada ya kumhoji, mke wake alikiri kuwa alipewa na mwanaume aliyemtaja kwa jina la Hussein.
Alisema Mtunda aliamua kuchukua hatua hiyo ya kumhoji kwa kuwa alijua mke wake hana uwezo wa kuzipata khanga kutokana na hali ya kifedha waliyonayo.
Alisema baada ya mahojiano hayo, aliamua kuongozana na mke wake hadi kwa Hussein na walipofika nyumbani kwake na kumuuliza juu ya tuhuma hizo, alikataa.
Hata hivyo, alisema baada kukataa, mtuhumiwa huyo aliamua kumpigia kelele za mwizi ambazo zilijaza wakazi wa eneo hilo na kuanza kumshambulia kwa silaha mbalimbali.
Alisema baada ya kuuawa, ndugu wa Mtunda walifika eneo hilo na kuanza kumshambulia Hussein kwa kipigo na kumsababishia majeraha mwilini.
Alisema kwa sasa mtuhumiwa huyo amelazwa chini ya uangalizi mkali hospitali ya Amana na kwamba upelelezi zaidi juu ya tukio hilo unaendelea.
Katika tukio lingine, mwili wa mwanaume ambaye hajafahamika jina lake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 na 35, umekutwa kandokando mwa barabara ya Ubungo ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali mwilini.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Bw. Jamal Rwambow, alisema jana kuwa mwili huo ulionekana juzi asubuhi kwenye barabara ya Ubungo iendayo Msewe, jijini.
Kamanda Rwambow, alisema uchunguzi juu ya kifo cha mwanaume huyo bado unaendelea na kwamba kwa sasa mwili huo umehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala.
* SOURCE: Nipashe