Mhindi umetoa kitu nisichokifahamu

Mhindi umetoa kitu nisichokifahamu

nyabubu

Member
Joined
May 1, 2017
Posts
32
Reaction score
23
Wadau wa kilimo, kama kuna mtaalam anafahamu hichi kilichopo kwe picha ni kitu gani, atupatoe elimu kidogo, maana nimeikuta shambani kwangu, imenistua sana maana, sijawahi kukutana na product hii..

Ukichunguza kwa karibu ni kama vimifuko ambavyo kwa ndani vina unga laini sana mweusi.. Mfano wa unga wa ngano mweuzi wenye nyuzi nyuzi.

Asante

IMG_20190425_173416_7.jpeg
IMG_20190425_173442_3.jpeg
IMG_20190425_173446_5.jpeg
 
Mtafute BW. Shamba kama anapatikana karibu anaweza kuielezea kitaalamu....me nilijaribu kumuuliza bibi kilimo akawa yupo shallow akaomba nimpe sampo aipeleke maabara sijui...hakurudi tena kuleta majibu
 
Ni ugonjwa wa kawaida sana kwa mahindi wala haushtui we ukulima umeanza lini mkuu mpaka hicho kitu kinakushangaza
 
Hiyo ni fungal disease iitwayo MAIZE SMUT, Unasababishwa na fungus waitwao Ustilago maydis, kupitia michibuko katika mmea fungus hushambulia cell za mmea na kusababisha kuwa hivo.
 
Dah! Pole sana mkuu. Una umri gani?? Umesha oa/olewa? Ningelikuwa ni miye ningeliliacha hapo hapo hilo shamba nihame mkoa. Hiyo ni sawa na mmea unaoitwa "The Black Tulip" Ukiuona tu ni kifo. Hapo na weye kwishaaaa. Muone mshana jr akupe utaalam
 
Dah! Pole sana mkuu. Una umri gani?? Umesha oa/olewa? Ningelikuwa ni miye ningeliliacha hapo hapo hilo shamba nihame mkoa. Hiyo ni sawa na mmea unaoitwa "The Black Tulip" Ukiuona tu ni kifo. Hapo na weye kwishaaaa. Muone mshana jr akupe utaalam
[emoji23][emoji23][emoji23]....Asee acha mchimba huyo kijana mkwara
 
[emoji23][emoji23][emoji23]....Asee acha mchimba huyo kijana mkwara
Mdanganye mwenzio ajikute morg bila sababu. Kwani kifo kizuri?? Nimempa ushauri wa kukimbia hilo shamba lina mzimu hapo
 
Huo ni ugonjwa kwenye zao la mahindi unaitwa Corn Smut unasababishwa na Fungus wanaoitwa Ustilago Maydis
Husambazwa kwa njia ya hewa, umwagiliaji, kinyesi cha wanyama kam ng'ombe akila masalia ya mahindi yaliyoshambuliwa, mbolea ya samadi kama mifungo imelishwa chakula kilicho contaminate hawo fungus huenezwa kupitia Spores(ungaunga) unaokuwa kwenye guzi la mhindi(Uvimbe) ukishakauka.
Favourable conditions( hali inayoruhusu usambazaji wake ni Winter (kiangazi) kipindi kirefu ch jua maana hukausha spores na kuweza kuruhusu kusambaa .
Spores zinauwezo wa Kukaa kwenye udongo miaka 5-7 .
Namna ya kuzuia
Hakuna dawa yoyote ya fungus inayoweza kutibu bali kuna njia za kupunguza asali na kuondoa Kabisa Ugonjwa kwenye shamba
Nazo ni:
Kuharibu na kuteketeza mahindi yaliyoshambuliwa kabla ya kukauka na kupasuka.
Kupungu injury kwenye mizizi ya mimea mana spores zinazokaa kwenye udongo huathiri mmea kupitia michubuko ya mizizi.
Kuchoma na kuteketeza masalia ya mmea iliyoshambuliwa.
Kutotumia masali yaliyo shambuliwa kama malisho ya Mifugo ili kuepuka usambazaji wake
 
Back
Top Bottom