Wakuu na Tatizo kubwa kuliko yote na ambalo nilisha wahi kulitolea maeleo kwenye jukwaa la Biashara ni hili hapa
1. MFUMO WA UCHUMI WETU
Ujamaa wetu, ilichangia sana kutufikisha hapa tulipo, na mfumo wa kijamaa mara zote unalemaza hadi akili na unafanya watu tuamini kila kitu ni serikali ndo inatakiwa kufanya, cheki nchi kama Kenya walio anza na mfumo wa Kibepari, wao hawana matatizo kama yetu, Vijana wana jijairi bila tatizo lolote
2. WAZAZI WETU
- Wazazi wanachangia asilimia kubwa sana kuharibu feature za watoto wao bila kujua lakini, Mdao hapo juu pamoja na kwamba amesomea UJASIRIMALI, lakini wazazi wake Tangia akiwa mdogo walikuwa wana mwambia asome aje kuwa Meneja, Mkrugenzi, Rubani wa Ndege na kazalika, Hii ikakaa kichwani mwake na alisoma kwa bidii ili aje kuwa Mkurugenzi au Menbeja
HAKUNA MZAZI HATA MMOJA ANAYE MHIMIZA MTOTO WAKE ASOME AJE KUWA MFANYA BIASHARA MKUBWA KAMA MENGI,
3. JAMII INAYO TUZUNGUKA/MARAFIKI/MAJIRANI
Mkuu sucess is Genetic mkuu kama MAJIRANI, WAZAZI, MARAFIKI NA NDUGU wote ni Wafanyakazi uwezekano wa wewe kuja kuwa Mfanya biashara ni mdogo kwa sababau umekua ukiwaona wakienda kazini wakipiga tai zao, wakilietwa na magari ya Kampuni/serikali, hii inakuwa inakuvutia sana na wewe kutamani siku moja uje kuwa kama wao
CHUKULIA MFANO WA WAHINDI: Hawa watu watoto wao wanakuwa wakiwaona Wazazi wao wanashinda madukani. Marafiki zao wazai wao ni wafanya biashara, Majirani zao wote ni wafanya biashara, HAPA AUTOMATICALY WATOTO NAO WATAKUJA KUWA WAFANYA BIASHARA WAZURI, ndo maa huwaoni wakitafuta kazi kama WABONGO,
4. VYUO VYETU/SHULE ZETU
Hapa napo elimu zetu na cyuo vyetu vimekaa ki theory zaidi, na hata walimu nao wanasisitizi watoto wasome waje kuwa Wakurugenzi, so ni lazima watoto waje kuwa wafanya biashara
SO WAKUU DHANA YA UJASIRIMALI INATAKIWA IANZIE MBALI SANA NA SI VYUONI PEKEE