Mhitimu wa chuo apigwa na kuvuliwa nguo, sababu ya Tsh 5000

ISENUKA

Member
Joined
May 25, 2014
Posts
81
Reaction score
10
Katika hali isiyokawaida mwalim mtarajiwa aliyesomea katika chuo cha Tumaini Makumira ngazi ya degree, amejikuta akipokea kipigo kutoka kwa mwananchi mwenye hasira kali, ikiwa sababu kubwa ni kudaiwa Tsh 5000, akitoa maelezo mwalim huyo akiwa hospital anadai alipewa hyo pesa kutoka kwa mzazi huyo ili amfundishie mwanae.

Na baada ya mwalim kuona mwanafunzi hafiki sehem ya mafunzo,ndipo alipoamuwa kuachana nae na kuondoka kwenda Songea kwa mjomba wake, aliporudi tu ndipo mzazi wa mwanafunz akadai pesa yake, mwalim huyo alimuaidi kuwa ampe siku 4 atakuwa kasha rejesha kiasi hcho.

Mzaz alipoona siku ya ahadi imewadia alimfuata mwalim huyo,ndipo mwalim huyo akasema atampa akisha ajiriwa kupitia pesa ya kujikimu na atamtumia kwa njia ya mtandao, ndipo mzaz huyo alipopandisha hasira na kumvamia mwalim huyo na kisha kumpiga na kumvua shati na viatu vyenye thamani ya 45,000/=,hadi muda huu naingia JF mwalim bado yupo hospital kwa uchunguzi zaid wa kiafya na mzaz anashikiliwa na polisi.
 
Mh! walimu mtaajiriwa tu ajira zenu zipo.
 
Serikaliiiiiiii toeni ajira walimu wanaadhirika huku mitaani.
 
Ameaibisha secta ya ualim. Kwanza ni muongo, halafu tapeli. Kwa nini aweke ahadi zisizofikiwa? Aliomba hela amfundishe mwanafunzi, akapewa zikawa nauli ya kwenda kwao. Iwe aliweka vocha akaomba mahela kwa mwingine akakimbilia kwao. Huko ndo huyo mwanafunzi alikuwa?

2. Aliporudi, akaahidi kurudisha fedha ya watu baada ya siku 4, jambo ambalo hakulitimiza.

3. Alipofuatwa tena, anajibu kwa jeuri, ngoja niajiriwe nitakapopewa hela ntakutumia kwa mtandao.

Kwani ulizipewa kwa mtandao?? Hiyo ni dharau sana tu. Akakuta mtu mwenyewe hana simile, akambamiza. Nasema, ka anayo akili kidogo, atoke huko hospitali akaombe radhi na kesi aifute mwenyewe polisi.

Sio hivyo, aombe uhamisho kwani keshaleta uadui kijijini /mtaani kwake.
 
Duh!kweli ualimu ni laana,yani mtu anakosa hata buku tano!

Mkuu ualimu sio laana!

Wewe najua ni mtaalamu wa economics, so nitakachokiongea utakielewa vizuri kuliko watu ambao hawajasoma hilo somo.

Kuna aina ngapi za ulipaji wa madeni?

Huyu mwalimu alishindwa kwenda kukopa kwingine ili alipe kwa huyo mzazi?

Ila kwa upande mwingine naona mzazi alikuwa sio economical, yani niwe nakudai buku tano halafu chini umevaa 45k, kwanini nijitakie R.B ya kukupiga???

Wote wawili ni wabovu upstairs!!
 
Anaitwa nani nahisi anaweza akawa ni mshikaji wangu maana na mm nimemaliza Tumaini Makumira ebu niambie naweza kumsaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…