Mkuun unafurahisha sana, Bila shaka Utakuwa Umesoma MZUMBE UNIVESITY kitengo cha BBA-ED, Mkuu ni kweli kabisa hiyo Kozi ni mahususi kwa ajili ya Kujiajiri mwenyewe, Tatizo lina kuja kwamba Spirit ya Mtu kujiajiri inatakiwa ujengwe tangia mwanzo na si Chuoni, Hii inatokana na kuwa na mentality ya kuajiriwa tangu akiwa CHEKECHEA, SHULE YA MSINGI, SECONDARY NA HATA CHUO
Walio kuwa wamekuzunguka kuanzia Majirani, Marafiki na hata Wazazi wote wana weza kuwa ni Wafanya kazi sasa shughuli ndo inaanzia hapo,
Mkuu mimi sikushauri uajiriwe, na kwa sababu wewe umedai ni mtalamu wa Komputa unaweza tumia elimu ya Ujasirinali uliyo pata kutafuta Mtaji,
Na Mkuu UNAPO KUWA NA MAWAZO YA KUJIAJIRI HUKU UKITAMANI AJIRA ZA KUAJIRIWA HUTAKAA UFANIKIWE KAMWE NA UTAKUWA UNAJIDANGANYA BURE, Mkuu kama Umedhamiria kujiajiri inabidi uweke Pamba masikioni na Uvae Miwani ya Mbao,
Na unatakiwa kufanya haya
1. Ikibidi Ondoa namba za Rafiki zako wote ambao unazania watakufanya ndoto zako za kijiajiri zisifanikiwe
2. Badilisha namba ya simu ikibidi
3. Badilisha Marafiki ikibidi, anza kutafuta marafiki wajasirimali, na sio wafanya kazi
4. Epuka kuomba ushauri kwa ndugu jamaa na marafiki kuhusu kujiajiri labda tu unao waomba Ushauri ni Wafanya Biashara