bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,213
- 2,938
Mwanamke anayefanya kazi ya kuhudumia mazishi, anayejulikana kwa jina la Mary, nchini Ghana alinukuliwa akisema kuwa mara nyingi huhisi furaha anaposikia kuwa mtu amefariki dunia.
Mary alisema anahisi furaha kwa sababu tukio hilo humpa kazi na kumsaidia kuingiza kipato.
Alisema kuwa baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka kadhaa, ameelewa kwamba kifo ni sehemu ya maisha na hakiepukiki.
"Mama yangu akifariki nitaelewa. Nikijifungua mtoto halafu akafariki, nitaelewa. Nikilala leo na nisiamke kesho, nitaona hilo ni jambo la kawaida," alisema Mary.
Mary aliongeza kuwa mtu anapofariki yeye ndiye atakayepata kandarasi ya kusimamia mazishi ya marehemu, hivyo yeye huwa anafurahia kwa sababu tukio hilo linampatia kipato.
Mary alitoa kauli hiyo ya kushangaza mwaka 2023 wakati wa mahojiano na kituo cha Ewiase Mu Nsem TV, akieleza kuwa kama ilivyo kwa taaluma nyingine yoyote, yeye pia huomba apate kazi ili aweze kujipatia kipato na kujikimu kimaisha.