Umelipa ada, umegharamia vingi ila hesabu hivyo umevitoa sadaka.
Kama kashindwa kukusikiliza ukisema kitu fulani hupendi, yeye akaamua kukifanya tena. Tayari ni dharau hizo inaonesha hataki aende unavyotaka wewe, sasa jiulize huo uchumba wa kujichunga sana ili mwenza asije ona kasoro akasitisha ndoa. Ndo anafanya namna hiyo, je akija kuipata hiyo ndoa kawa amepata kila uhakika wa kuwa mke wa mtu. Ataacha kukusikiliza mangapi? Kama jambo dogo hilo linamshinda.
Kimtazamo wangu na si lazima uukubali, huyo si mke wa kuoa. Kama kafikia umemwonya na haachi maana yake huwezi mrekebisha. Usijipe tabu ndugu anua nanga, ondoa meli ukaweke nanga bandari nyingine.
Akikutana na huyo jamaa jua ataliwa kama kafikia kumwambia kamlowesha, hii maaana yake anajiona yupo huru zaidi akiongea na jamaa. Vipi akikutana naye?
je unaweza kuzuia hilo? Maana mtu mzima hachungiki ukumbuke hutakuwa naye kila wakati, andika maumivu hapo.
Kumpiga mikwara huyo jamaa haisaidii kitu kama mwanamke hakusikilizi, ndiyo maana nikakwambia hesabu gharama zako ni sadaka na Mungu atakulipia kwa kukujalia mchumba mzuri