Mkuu, kama ni kweli uyasemayo naomba nikushauri jambo kitaalamu, huyu mwanamke sio mke na nikwambie tu mshukuru Mungu wako, ujue watu wengi huumia kwa kutokukubaliana na hali, hii imegawanyika sehemu nyingi, kuna watu the way walivyo ni kutokana na ubishi wa kutokukubali hata kama akiambiwa ukweli, kwa jumla huyo unaedai mchumba wako ni malaya wa kutupwa, tena muogope kama ukoma. Maana ikiwa hutakubali kuwa umeshapoteza mapema basi jiandae kujinyonga kama sio kufa kwa pressure, pesa inatafutwa, ila furaha ya moyo haiuzwi popote, ni kweli ulimhudumia lkn waweza pia kumlisha mbwa wako mwenyewe na siku akakudhuru pia, haya yapo, mapenzi ndivyo yalivyo wala usione kama ni jipya kwako. Ikiwa mwanamke wako ana udhubutu wa kumwambia mtu eti nimeloa, dah. Halafu wanawake kuweni makini, huu mtindo wa watu kujifanya wanajua mapenzi ni storry tu kama za kina shigongo, wengi mnapotea na kuvunja ndoa zenu pasipo kujielewa, iweni na maarifa ili msiangamie.