Mimi nina mchumba ambaye kwa sasa ni mwezi wa 5 nipo naye. Kazi zangu ni za safari safari sana, so kila wakati nakuwa safarini......mchumba wangu amemaliza chuo mwaka wa 2 sasa hana kazi. Yeye ana muda mwingi sana so anakuwa home.... ila ni muda sasa naona amezoeana na member mmoja humu ndani....huyo member akianzisha thread huyu mchumba wangu analike na anachangia sana na huwa akisoma anasoma anacheka mpaka machozi yanamtoka muda wote akiwa nami anajisahau anaaanza kusoma threads za huyo jamaa baadaye nikamwambia mi sipendi anavyokuwa occupied sana na huyo jamaa mpaka anajisahau anasema "ila wanaume wengine bwana yaani ukikaa na huyu kaka itakuwa mtu hata stress .....
huyu dada mimi nlishamhudumia sana chuo mpaka amemaliza ni mimi nlikuwa natoa ada kumwonesha tu kuwa nipo serious pesa za kutoka kwa wazazi wake alikuwa anatumia kufanyia mambo yake na nilimruhusu nikamwambia basi aangalie kama anaweza zifanyia kazi flan ya kuzalisha, she didnt do anything progressive with the money.
Poole sana Bwana chizi..lakini ningependa urejee yafuatayo na kujibu maswali ili nipate Mwanga wa kukushauri vizuri.
1.Kwasasa ni mwezi wa TANO upo nae!
Swali:Kwa ubize uliinao umewahi kutenga mda wa kutosha kukaa nae nyumbani walau wiki moja!?
2.Amemaliza chuo miaka miwili ilopita
Swali:Miaka miwili ni miezi 24,ukitoa mitano mlokaa pamoja,miezi 19 ilobaki alikuwa wapi na alijishughulisha na nini!?
3.Unasafiri sana,hivyo mda nwingi anakuwa mpweke nyumbani na Hana kazi ya kumkeep busy
Swali:Unahisi huu ni mfumo salama wa maisha ya majaribio ya ndoa?
4.Umegundua anavutiwa na member humu ndani..na uhusiano wao unatishia afya na uhai wa mahusiano yenu.
Swali:Umemlaumu sana Member (jina umelihifadhi)lakini kwa maelezo yako inaonekana mchumba ndo Chanzo cha ukaribu wao,huoni kwamba kumchukia na kumlaumu huyu member bila kushughulikia udhaifu wa mchumba wako ni uchokozi na kutafuta uadui kwa member asiyekuwa na hatia?(mana pengine hajui kama mdada ni mchumba wako?
5.Umemhudumia sana wakati akiwa chuoni
Swali:Wakati unamhudumia ulijiridhisha kuwa anauhitaji na kuuthamini msaada wako?
Ulijiridhisha anakupenda,yupo tayari kuwa mkeo na ndie mwanamke sahihi kwako au ulifanya kwasababu unauwezo ama ulihisi ulifanya hivyo ndo atakupenda zaidi!?
6.wakati unamhudumia hakutumia frusa ya fedha ya wazazi kwa faida.
Swali:Hukujifunza chochote wala hukugundua chochote!?
Ulimshauri nini bada ya kuona anakiuka miiko ya kujenga maisha ya badae ukizingatia tangu amalize chuo ni miaka miwili sasa hana kazi!?
Majibu sahihi ya maswali haya yatasaidi sana kukufumbua macho na ufahamu wa kufanya maamuzi sahihi.Kila la kheri Chizi Maarifa