Miaka 10 Daraja la Nyerere (Kigamboni), NSSF yakusanya Tsh. 150 Bilioni

Miaka 10 Daraja la Nyerere (Kigamboni), NSSF yakusanya Tsh. 150 Bilioni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekusanya Tsh. 150.04 bilioni kutokana na tozo za matumizi ya Daraja la Nyerere Kigamboni katika kipindi cha miaka 10 tangu lilipoanza kutumika Mei 2016.

1789984016370.png
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema hayo Jumatatu, Septemba 21, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi kati ya menejimenti ya mfuko huo, wahariri na waandishi wa habari chini ya uratibu wa ofisi ya Msajili wa Hazina.

Soma: Deni la Daraja la Kigamboni (Mwalimu Nyerere) litaisha lini?

Amesema mradi huo katika ujenzi uligharimu Tsh. 345.20 bilioni, zikiwemo Tsh. 328.74 bilioni za ujenzi na Tsh. 16.46 bilioni zilizotumika kulipa fidia kwa wananchi waliohamishwa kupisha ujenzi wa mradi huo.

“Mradi huo ulipangwa kurejesha fedha zilizowekezwa ndani ya kipindi cha miaka 30 na Juni 2026, NSSF ilikuwa imekusanya Tsh. 150.04 bilioni kutokana na tozo za matumizi ya daraja,” amesema.

Pia soma: Serikali yaomba muda zaidi kujibu kesi ya tozo Daraja la Nyerere (Kigamboni)

Katika kipindi hicho, amesema NSSF pia imetumia Tsh. 25.81 bilioni kwa gharama za uendeshaji na matengenezo ya daraja hilo huku mapato yaliyokusanywa yakiendelea kuchangia katika kurejesha fedha zilizowekezwa kwenye mradi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa hiyo kwa mwaka walikuwa wanakusanya Bilioni 15 na kwa mwezi ni Bilioni 1.25. Bas sawa
=============================

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekusanya Sh150.04 bilioni kutokana na tozo za matumi.jpg


Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekusanya Sh150.04 bilioni kutokana na tozo za matumizi ya Daraja la Nyerere Kigamboni katika kipindi cha miaka 10 tangu lilipoanza kutumika Mei 2016. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema hayo leo Jumatatu, Septemba 21, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi kati ya menejimenti ya mfuko huo, wahariri na waandishi wa habari chini ya uratibu wa ofisi ya Msajili wa Hazina. Amesema mradi huo katika ujenzi uligharimu Sh345.20 bilioni, zikiwemo Sh328.74 bilioni za ujenzi na Sh16.46 bilioni zilizotumika kulipa fidia kwa wananchi waliohamishwa kupisha ujenzi wa mradi huo. “Mradi huo ulipangwa kurejesha fedha zilizowekezwa ndani ya kipindi cha miaka 30 na Juni 2026, NSSF ilikuwa imekusanya Sh150.04 bilioni kutokana na tozo za matumizi ya daraja,” amesema. Katika kipindi hicho, amesema NSSF pia imetumia Sh25.81 bilioni kwa gharama za uendeshaji na matengenezo ya daraja hilo huku mapato yaliyokusanywa yakiendelea kuchangia katika kurejesha fedha zilizowekezwa kwenye mradi.​
 
Kwa hiyo kwa mwaka walikuwa wanakusanya Bilioni 15 na kwa mwezi ni Bilioni 1.25. Bas sawa
Miaka ya mwanzo walikuwa hawafiki hata 1b kwa mwezi. Magari yalikuwa machache na Ferry palikuwa vizuri wengi wanaotoka Geza,Mjinwema etc walikuwa wanapita Ferry. Miaka ya karibuni magari yameongezeka na magari ya Kigamboni asilimia 95% yanatumia daraja.
 
Back
Top Bottom