Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE NDAISABA ASHIRKI HAFLA YA MIAKA 10 YA CRDB KUTOA HUDUMA ZA KIBENKI KUPITIA MAWAKALA
Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndaisaba George Ruhoro tarehe 08 Mei, 2023 alishiriki Hafla ya kuadhimisha miaka 10 tangu CRDB walipoanza kutoa Huduma za Kibenki kupitia Mawakala ambapo Hafla hiyo iliandaliwa na CRDB - Ngara na kuwahusisha Mawakala wa CRDB Wakala waliopo Ngara
Ndaisaba amewapongeza CRDB kwa kuendelea kuwa wabunifu katika kutoa Huduma za kifedha kwa Umma, lakini nimewaomba wafanye ubunifu ili Mawakala wa Tanzania hususani Ngara ambapo wanapakana na Nchi za Rwanda na Burundi kuweza kuwahudumia wateja wa CRDB wanaotoka kwenye mataifa hayo ili kuchochea ukuaji na mahusiano ya kibiashara baina ya nchi hizi kwani kwasasa Huduma hii haipo na Wananchi hao hupata shida hususani baada ya masaa ya Benki
Mbunge Ndaisaba ameipongeza sana Serikali ya CCM chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutilia mkazo suala la Ujumuishi wa Huduma za Kifedha (Financial Inclusion) kwani imechochea sana ukuaji wa sekta za Kibenki na kuongeza Ajira kwa Vijana na Mapato kwa Serikali
Kabla ya Huduma hizi kuanza watu walilazimika kusafiri umbali mrefu sana kutafuta Huduma ya Fedha, Baadhi ya wagonjwa walipoteza maisha kwa kukosekana pesa kwa haraka kutokana na ugumu wa kupata Huduma za kifedha
Mawakala wa CRDB wamekuwa na mchango mkubwa sana katika kuwezesha Huduma zote zinazotegemea fedha.
#TulipoWapo