Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Hili janga la kuvurunda mwanzo ajira wakati mpunga unapatikana kirahisi linatusumbua wengi. Hasa mikopo ya kufuata mkumbo mwisho inakuja tutafuna!
Kwa watumishi wenye nafasi ya kujihusisha na kilimo au ufugaji hasa tulio vijijini tuingie huko, fedha ya mshahara itaonesha matunda yake. Mambo mengi yatakua rahisi mfano sehemu kubwa ya chakula itapatikana moja kwa moja bila kutazama unachopata kazini.
YOTE KWA YOTE TUWE POSITIVE!!!
 
Mkuu uko Kijiji gani boss, tupeane fursa
 
πŸ˜„πŸ˜„Basi mrudishie huyo baharia vyote alivyokuhonga, haiwezekani wewe upende kuppkea halafu ushindwe kutoaπŸ™ŒπŸΌπŸ€”
Hakuombwa. Hapo ndio shida inapoanzia
 
Hii ni kama alert asee.
Mwaka jana nikiwa na umri kama wako nilibahatika kupata job flani ya hela ya maana ,yaani nilipiga dollar balaa.
Leo hii mwaka mmoja baadae sina ninachomiliki zaidi ya hii simu na geto la 50k ,kazi imeenda na Corona.
Lakini nimeamka sikati tamaa
 
Ulikuwa 21 Kama wangu wa zamani au 31 wa Sasa?
 
just forgive yourself bro! Naamini kuwa hizi ni hatua za maisha na pia zinakufanya uthamini jasho lako. Mie Kama wewe kila nikifikiria pesa nilizochezea 2008-2011 natamanigi nijifukie ardhini. Mie tofauti na mshahara I was getting up to 3 Million Tsh per month naishia kuwapikia ndugu wa mume. Yaani hata kacheni ka dhahabu sikununua (haha haaa). Anyways yote heri nilikuja kujitambua immediately after that yaani hadi kufika mwaka 2014 ni mtu mwingine kabisa. Namshukuru Mungu nimepata nafasi nyingine. Maisha yanaendelea. I chose to be wise!
 
Hongera kwa kuishinda hiyo hali
 
Mfumo wa ndoa yenu nimeupenda sana watu 4 tu, na hamna hata senti 5 kutumika.. Lakini mara nyingi ndoa za hivo huwa zinadumu kuliko hizi za gharama
 

Hujachelewa mkuu kwanza nikupongeze kwa kushtuka mapema.Mimi nilidhani hiyo tabia ni kujiendekeza lakini nimegundua katika hiyo stage ya kushika hela umri huo ni ngumu kuepuka vishawishi,miaka 8 iliyopita nilipata kazi arusha Mara tu baada ya kumaliza stashahada ya juu katika fani ya uhasibu nikiwa na umri wa miaka 24,Ukwel kazi ilinilipa vizuri kiasi ningeweza kufanya mambo Makubwa kwani kipato kilikua kinaruhusu,kama unavyojua totoz za kijenge,mushono,pinpoint bila kusahau babilon na maeneo mengine ya Arusha ilikua hatari,kuchukua fastjet kwenda Dar es salaam kula raha kitu cha kawaida sana,kupandisha ndege totoz kuja arusha kitu cha kawaida ,mitungi ndo usiseme .Mimi mwenyewe nilikua nakaa nakumbuka nahisi ni akili yangu ile au nilirogwa?lakini sasa nimeamua kusahau yaliyopita na kusonga mbele na maisha yanaendelea japo mambo si mazuri sana kama wakati ule....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…