Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Mkuu pole sana ila bado una nafasi umeshtuka mapema.

Me nilichokigundua mpaka leo kwa wa tz wengi wanapopata kazi huwaga hawana vision tena Baada ya pale,ndio maana tz mpaka leo watu wake bado wanaangaika kila siku wachache watakao jitambua kama wewe wanatoboa.

Sio kwamba uku pata washauri mkuu ,wewe kama wewe unatakiwa uwe na vision ya maisha yako kama ulivyoweza kutoboa mpaka umepata kazi umefika hapo ulipo,ulivyofika hapo ulikuwa na washauri?

Usipende sana kujilinganisha na wengine hao unaweza ukakata tamaa focus na maisha yako huku ukiwa unapanga malengo yako tu,na jifunze kuwa mbahili saizi kwenye kutafuta.

Hali uliyokutana nayo iko kwa wantanzania wengi ndio akili zetu hizo ,ndio maana mpaka leo raia tupo busy kutafuta halafu bado maskini.

Mkuu nakushauri hiyo kazi usiache mpaka mwenyewe waseme wewe basi kuendelea baada ya hapo amia kwenye biashara zako.

Maisha yana kuwa easy sana kama unakuwa unajiwekea malengo kwa kila hela utakayo ipata,ndio maana wazungu wanatuzidi,wazungu wengi wakipata kazi tu wanajua tayari vitu gani wanahitaji muhimu kuwa navyo kwenye maisha yao,kitu kama mke ,nyumba,kiwanja biashara za kufanya.sio sisi ,sisi tunatumia kinaisha kesho tunaanza upya.

Hongera pia mkuu umejitambua mapema,wengine mpaka anastafu ndio anaanza kujilaumu nilikuwa nachezea hela kumbe.

Vijana wengi wakipata kazi wanaangaika kwanza na simu za milioni 2,3. Mpaka unashangaa huyu hela yake hana matumizi mengine hizo simu za gharama utanunua tu fanya mambo ya msingi kwanza jipange kimaisha kwanza ,ukimshauri hakuelewi na hela anazo utamwambia nini?

Kwa sababu usipo fanya vitu vya muhimu saizi kwenye maisha unakuwa unajichelewesha wewe mwenyewe maana baadae utatakiwa uwenavyo na wewe wakati huo huna hela,utabaki tu kujilaumu.






Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi na mwaka huu natimiza miaka 21 ya utumishi nina umri wa miaka 37 tu nimeajiriwa nikiwa mdogo mno umri wa miaka 17 tuu nikabahatia....aisee yangu mm makubwa mno nimepitia mengi mno nimeona mengi mno tena ya kutisha sana, maisha ni safari ndefu naweza sema nita staafu nikiwa bado nguvu ninazo za kutosha nina miaka 10 tuu mbele ya kustaafu hii kazi...Labda waniongezee mkataba wakiniongezeea nakataa sitaki mana nisije kufa bure......
 
kazi gani hiyo uliyoajiriwa ukiwa na umri wa miaka 17 mkuu?
 
Maisha haya! Ila imekua safi sana kujishtukia mapema mkuu bado una umri wa kufika unapotaka. Ila Mungu huwa hakupi wala hakunyimi vyote yani wakati unasema umechoma hiyo hela kwa kukosa mshauri au msimamizi ye amekubariki na huyo mwanamke makini, ni vema kushukuru kwa hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa sikufanya kosa, kosa ni kurudia kosa! Bora umejitambua muda haujaenda sana. Nakutakia la kheri kwenye maisha yako baada ya kujipanga upya!

 
Nina washkaji waliofanya hayo makosa mimi sijafanya ... nilipata ajira soon tu nilivyomaliza chuo mwaka 2017 mwezi wa 11 nilifanya interview ya kwanza mwaka huohuo Mungu sio Paskali mayalla nikapata ...kama unajua kazi zetu hizi za majitoleo ( Mwalimu ) mshahara sio mkubwa yani hizo posho zako tu umeuzidi mshahara wangu wote πŸ˜‚ ( life’s not fair) ukiangalia walimu wako wengi mtaani lol salaale unajikuta umesema ndio nimekubali hata kabla hajamaliza kutaja kiasi atakachokulipa ...

To cut the story short nilikutana na manguli wa Taasisi watu wana miaka takribani 10 mpka 15 ila hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kujenga... wanaomiliki ndinga ni kama hizi za kutangazia matangazo ya dawa za asili sokoni ( mikweche haswaa ) ... na stori ikawa ni hiyo kwamba kumiliki nyumba ( kibanda) ni sawa na Ngamia kupita kwenye tundu la sindano ( haiwezekani ) mzee wa mlengo wa kulia ikabidi ni pige hesabu bila kutumia mshahara wangu kwa mwaka napata mil 7 hivi ina mana kwa miaka miwili mil 14 ...

kweli bwana nikawa nakula kwa mwezi 90000 tu ndio tisini elfu hujakosea ( kula katikati ya wiki unakula shule asubuhi na mchana ) kodi unalipiwa na shule ikawa ndio utaratibu wangu baada ya kipindi cha mwaka nikapiga msingi na nikaacha na tofari mwaka huu nimeipandisha mpka renta jumla kama mil 8 hivi ... ninapofanya kazi hakuna anaejua wala kuhisi mana hata picha nikipiga na save iCloud ...

Bila ya hii KORONA ningepauwa tena na Roman versatile basi tu ... usiache kazi mzee biashara mueke mkeo mana umesema amekuzidi maarifa
 
Hongereni wakuu kwa kila hatua mnazopiga tupo pamoja na poleni kwa maswaibu mbali mbali yanayojitokeza ktk maisha kutokana na kujisahau.
Binafsi ningependa kutoa ushauri,kitu starehe,yaani pombe + mademu ni adui mkubwa sana wa maendeleo.ukitaka mafanikio ipende pesa na uieshimu na rafiki wa kweli ni pesa yako ,tunza pesa ,tunza pesa kamwe haitakutupa.

Anasa ni mbaya sana kwenye maisha,tuwape elimu walio chini yetu wasije situka kumekucha
 
Kama nakufahamu mdomo wangu..
 
Mwenzako mi mpaka leo najuta kwanini sikuenda kusoma Diploma vyuo vya ufundi nikaenda Form 5. Mkuu, hili ntajilaumu maisha yangu yote.

Anyway, maji yameshamwagika. Fresh tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…