Miaka 12 ya Samaki Samaki, mjue "Kalito Samaki"

Miaka 12 ya Samaki Samaki, mjue "Kalito Samaki"

Mla Bata

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
7,841
Reaction score
17,491
Ni miaka kumi na mbili (12) tangu kuanzishwe migahawa hii maarufu hapa bongo, kwa ambao washapata huduma za samaki samaki watakuwa mashahidi juu ya ubora, huduma nzuri na kikubwa ubunifu unaotumika kutoa huduma zao.

A man behind all these creativity sio mwingine bali ni Carlos Bastos ama "kalito samaki" kama wengi wanavyomfahamu. Jamaa ni muhispania aliyeishi bongo miaka mingi akiwa ni mtoto pekee kwenye familia yao. Kalito ana watoto watatu, wawili akiwa amezaa na mbongo huku mmoja wa mwisho akiwa amezaa hivi karibuni na muhispania mwenzake.

Licha ya kuwa muhispania kalito ni muabudu mzuri wa tamaduni za kitanzania ambapo mara nyingi utamkuta kavaa kimasai au msuli kama mtu wa pwani, Pia jamaa ni mtu wa watu sana ambapo muda mwingi hujichanganya na wateja zake kitu kilichompelekea kutengeneza marafiki wengi hasa wasanii.

Mnamo mwaka 2014 kalito aligundulika na melanoma (skin cancer) kwenye jicho lake la kushoto hali iliyompelekea kupoteza matumaini ya kuishi kabisa.

"Hii ni aina ya kansa , inayotokea mara chache. Kilikuwa kipindi kigumu sana kwangu tatizo la kansa sio kwakuwa iko eneo moja itabaki hapo tatizo ni kuwa ina uwezo wa kusambaa mwili mzima na kwa kawaida ikifikia hatua hii una kufa”

Alinukuliwa wakati akihojiwa na mtangazaji maarufu hapa bongo.

“Ile hali ya kuwaza muda wowote utakufa ilibadili sana maisha yangu na kunifanya niwaze tofauti nikaanza kujifunza vitu vipya ni kwa kiasi gani ili kulinda afya yetu tunatakiwa kula vizuri
Nimejifunza kufurahia kila wakati ninaopata kwakuwa sijui ni lini itakuwa siku yangu ya mwisho maisha yangu yakabadilika na sasa nimekuwa makini zaidi na maisha pamoja na ninayoyafanya”

Kalito aliamua kurudi kwao hispania kwa matibabu ambapo alifanyiwa operesheni ya kuondoa jicho la kushoto ambapo akaja na style ya kuvaa kitambaa cheusi (patch) kwenye sehemu ya jicho lake.

Ukiacha maisha yake binafsi Kikubwa kilichonifanya nimzungumzie huyu jamaa leo, ni ile roho ya upambanaji aliyokuwa nayo na ubunifu wa biashara ambapo kiukweli ni jambo la kujifunza. Kuna migahawa mingi sana bongo lakini mgeni huyu ameteka soko na kutengeneza jina kubwa kwenye biashara ya chakula na vinywaji.

Hili ni jambo la kujifunza kwa vijana na watu wanaoamua kujiajiri kuwa kitu chochote unachofanya kinahitaji ubunifu na focus kwenye kufanikiwa.

Wengi wanaweza kudhani jamaa alianzia hapo juu kwenye kumiliki migahawa lakini kiukweli jamaa alianzia chini kama Barman kwenye mgahawa wa CHUI BAY sasa ukifahamika kama Capetown fish market, alihudumu hapo kwa muda kadhaa kabla hajaanza kumiliki migahawa yake mwenyewe (the hustle was real).

Cha kujifunza ni kutokukata tamaa na kuweka malengo bila kusahau ubunifu kwenye kila unachofanya. Keep your dream alive, everything is possible for those who believe.

let's meet at the top. Cheers [emoji1635]
Inst-image-7.jpeg
Inst-image-6.jpeg
 
Tanzania nchi yenye kujaa fursa ambazo wageni huziona kwa wepesi kuliko Watanzania wenye nchi yao
Mguu wa msafiri huo, ndio maana wengine tumejiondokea kutoka Tanzania na tumekuwa wageni kwingine na wazawa huko tulipo nao wanatusema hivyo hivyo kwamba hawa watu hapa sio kwao lakini wana hustle na ku make it kuliko baadhi ya wazawa.

Ni mguu wa msafiri huo na mimi naukubali sana.
 
Mkuu kwenye kila comment yako uwa sikosi kupata chochote,hasa misamiati
 
Jamaa kaumwa jicho likatolewa, akaunganishia style ya U Pirate humohumo.

Hapo ndipo utajua maana ya "When you are given lemons, make lemonade.".

Don't cry for oranges.
Hahah for sure mkuu.
 
Mguu wa msafiri huo, ndio maana wengine tumejiondokea kutoka Tanzania na tumekuwa wageni kwingine na wazawa huko tulipo nao wanatusema hivyo hivyo kwamba hawa watu hapa sio kwao lakini wana hustle na ku make it kuliko baadhi ya wazawa.

Ni mguu wa msafiri huo na mimi naukubali sana.
Tunasema mguu wa kutoka siku zote una baraka mkuu.
 
Point muhimu

Back
Top Bottom