Miaka 150 kuanzia sasa

Miaka 150 kuanzia sasa

CARIFONIA

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2013
Posts
616
Reaction score
1,453
Miaka 150 Kuanzia Sasa


Miaka 150 kuanzia sasa, hakuna hata mmoja wetu anayesoma ujumbe huu leo atakayekuwa hai. Asilimia 70 hadi 100 ya mambo tunayoyapigania sasa yatakuwa yamesahaulika kabisa. Chora mstari chini ya neno KABISA.


Tukirudi nyuma kwa miaka 150 iliyopita, yaani mwaka 1872, hakuna hata mmoja wa wale waliokuwa wakihangaika kubeba majukumu makubwa ya dunia kipindi hicho ambaye yuko hai leo. Karibu sisi sote tunaosoma ujumbe huu tunaweza kupata ugumu hata kufikiria sura ya mtu yeyote wa enzi hiyo.


Tafakari kwa muda na fikiria jinsi baadhi yao walivyowasaliti ndugu zao na kuwauza kama watumwa kwa kipande cha kioo. Wengine waliwaua ndugu zao kwa ajili ya kipande cha ardhi, magunia ya viazi vikuu, sukari, au hata kiasi kidogo cha chumvi. Viazi hivyo, sukari, vioo, au chumvi walivyokuwa wakijivunia viko wapi sasa?
Inaweza kutuchekesha sasa, lakini ndivyo binadamu tunavyokuwa wapumbavu wakati mwingine, hasa linapokuja suala la nguvu au kutaka kuwa na umuhimu.


Nakumbuka siku zile nikiwa sekondari, jinsi watu walivyopigana na kufanya mambo yasiyofikirika ili tu majina yao yajumuishwe kwenye orodha ya wanafunzi waliotakiwa kuwa viongozi wa shule. Viongozi wa kawaida wa shule tu! Sasa ni miaka 18 tangu niimalize sekondari, hakuna hata mtu mmoja pale shuleni sasa anayekumbuka kuwa nilisoma hapo, licha ya umaarufu wangu wakati huo. Sasa fikiria ni nini kitatokea baada ya miaka 150?


Hata ukisema enzi ya mtandao itahifadhi kumbukumbu zako, chukua mfano wa Michael Jackson. Michael Jackson alifariki mwaka 2009, ni miaka 13 tu iliyopita. Fikiria ushawishi mkubwa ambao Michael Jackson alikuwa nao duniani alipokuwa hai. Mungu wangu, alikuwa kama mungu wa muziki. Je, ni vijana wangapi leo wanaomkumbuka kwa heshima, kama hata wanamjua? Miaka 150 ijayo, jina lake, hata likitajwa, halitakuwa na maana yoyote kwa wengi. Na hii ni kwa sababu alikuwa maarufu sana. Sasa fikiria kuhusu watu wengi ambao hawatawahi kujulikana ulimwenguni kama yeye.


Tuchukulie maisha kwa urahisi, hakuna mtu atakayetoka hai duniani. Ardhi unayopigania hadi uko tayari kuua kwa ajili yake, mtu fulani aliwahi kuimiliki, akafa, akaharibika, na akasahaulika. Hali hiyo hiyo itakukuta pia. Miaka 150 ijayo, hakuna magari wala simu tunazojivunia leo zitakazokuwa na umuhimu wowote. Tafadhali, tulia na uishi kwa amani!


Wacha upendo uongoze. Furahia wengine kwa dhati. Hakuna chuki, hakuna majungu. Hakuna wivu. Hakuna kulinganisha. Maisha si mashindano. Mwisho wa siku, sisi sote tunaelekea mahali pamoja—kaburini. Swali tu ni nani atafika huko kwanza, lakini hatimaye sote tutaenda.


CARIFONIA
 
Fact 99.99999999%
-Hakika mtakufa. Punguza kiburi cha uzima
-Usishii kwa majuto, jana na kesho ni nadharia na njia ya kutambua wakati lakini kiuhalisia havipo
-Leo ni zawadi itumie kufanya yaliyo bora zaidi
-Kabili tatizo kwa namna uwezayo hata ulikimbie litakuja kivingine
-Usijilinganishe na wengine
-Punguza makasiriko
-Uwe mwenye shukrani hata kwa kidogo ulichonacho
 
Ila mali zitakuwepo.
Naamini utajiri wa familia ya Dewji na Bakharesa utaendelea milele.

Na mimi nataka hivyo, kukomboa kizazi changu.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
"Tulia uishi kwa amani"

Tatizo linaanzia hapo, Utatuliaje na tumboni kuna njaa? 😀 utatuliaje na hauna uhakika wa maisha bora (chakula, mavazi na malazi) ya watoto na wajukuu zako utakaowaleta hapa duniani wakati utakapoondoka? Utatuliaje na hauna hicho kipande cha ardhi ili mkae kwa amani? Utatuliaje wakati unadhulumiwa haki yako/mtoto wako? nk. nk. Kabla ya hiyo miaka 150 kuna miaka 2,4,5... 10 ambayo inakuhitaji wewe na kizazi chako uvae,ule, upate makazi! Sasa bila hizo hekaheka unadhani utawezaje? 😀 BTW lawama apewe Adam na Eva na Kaini kwa kutuletea hizi hekaheka! Maana wao ndiyo mlango wa laana na hekaheka hizi za maisha. Tunapenda tukae kwa amani na kutulia, Ila laana inatulazimu kutafuta na kuishi kwa jasho!

All in all, Andiko zuri.
 
Back
Top Bottom